Makala za Freeman A. Mbowe, Mwenyekiti Taifa
13 Juni 2007
Waraka kwa Watanzania (4)
"...Viongozi wa vyama vya siasa wote, wanaotawala na wasiotawala, wana kila sababu ya kubeba lawama kwa taifa letu kukwama na kukosa mwelekeo. Kila mwananchi ni mbia katika lawama hizi. Kila Mtanzania, kwa nafasi yake ana mchango kwa njia moja au nyingine kwa hali yetu kuwa hoi kama ilivyo leo, pamoja na kuwa tumepishana kwa viwango..."
6 Juni 2007
Waraka kwa Watanzania (3)
"... Maafa ya mfumo huu hutokea pale ambapo waliopo kwenye madaraka ni viongozi dhaifu, wenye madhambi na hivyo waoga wa kuondolewa kwenye utawala. Hofu ya kupoteza madaraka hutamalaki.
Hali hii ikishajengeka, watawala hujiona salama zaidi ndani ya chama chao. Hutumia vibaya mamlaka ya serikali kujijengea uzio utakaofunika maovu yao. Hutumia fursa hii ya tofauti za kisiasa baina ya vyama kuhalalisha misingi ya kujenga chuki za kiitikadi, ambazo humomonyoa umoja wa kitaifa.
...."
30 Mei 2007
Waraka kwa Watanzania (2)
"... Bagenda, kwanza, anapendekeza kuwa Tanzania leo iwe na kile anachokiita “itikadi rejea”, akimaanisha itikadi ya ujamaa na kujitegemea ambayo yeye anaiona kama itikadi ya ukombozi dhidi ya mifumo gandamizi ya kibepari. Pili, anaainisha kuwa leo Tanzania hakuna hata chama kimoja cha siasa chenye programu iliyo wazi ya kutetea na kutekeleza itikadi ya ujamaa na kujitegemea. Anaongeza kuwa CCM wana itikadi hii vitabuni lakini sera zake za serikali zinakinzana na itikadi yake...."
16 Mei 2007
Waraka kwa Watanzania (1)
"...Rais wetu ana majukumu mengi na ni busara nimpe nafasi, kwa nia njema, atafakari kama akipenda, yale yote niliyoainisha kwenye tafakuri na nyaraka zangu kwake. Waraka wangu leo haumlengi yeyote kipekee, bali unakusudia kutoa ufafanuzi wa jambo moja la msingi. Hakika, kama yupo mwenye uelewa zaidi na mwenye kuamini maelezo yangu, leo ni ya kupotosha, ingekuwa busara ajitokeze na aseme, “Mbowe unadanganya.”..."
9 Mei 2007
Waraka wa sita wa Mbowe kwa Rais Kikwete
"...Nianze kwa kukupongeza kuhusu jambo moja la msingi. Kuelekea kupungua kwa safari zako za nje. Sina hakika kama kupungua kwa safari zako ni kwisha au kupungua kwa sababu za safari hizo au mshituko uliotokana na kudhihirika kupitia taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali juu ya matumizi makubwa ya serikali, tena nje ya bajeti..."
2 Mei 2007
Waraka wa tano wa Mbowe kwa Rais Kikwete
"...Mheshimiwa rais,
matumizi makubwa ya fedha yasiyo na mipaka, limekuwa ni jambo la kawaida kabisa kwa wagombea wa CCM wanaochuana ndani ya chama hicho chenyewe na dhidi ya wapinzani kuanzia katika udiwani hadi urais.
Hadi leo hii, bado tunajiuliza hivi ni mabilioni mangapi yaliyotumika kwenye kampeni za udiwani, ubunge na urais za chama chako na nini kilikuwa chanzo cha fedha hizo?..."
25 Aprili 2007
Waraka wa nne wa Mbowe kwa Rais
"...Kero kubwa za wananchi bado zinaendelea kuwa siri ndani ya serikali yako. Waziri mkuu wako anaendelea kwa kasi kulidhibiti Bunge na kukingia kifua ubadhirifu ndani ya serikali yako. Unayaona, unayajua, unakaa kimya, unayabariki. Ni wewe unayemtuma? Kwa nini tusiamini wewe ni sehemu ya ufisadi huu?..."
18 Aprili 2007
Waraka wa tatu wa Mbowe kwa Rais
"...Serikali ya Awamu ya Nne itaendeleza, kwa dhati, mfumo wa siasa wa demokrasia ya vyama vingi. Ushauri wangu kwa vyama vya upinzani kwa wapinzani ni kuwa wasiwe wepesi kutafuta mchawi kila wanaposhindwa uchaguzi. Badala yake nawaomba wajiulize kwa nini Watanzania wamewakataa kiasi hicho. Nina uhakika watapata jibu..."
11 Aprili 2007
Waraka wa pili wa Mbowe kwa Rais
"...Niruhusu, nitakapojadili hotuba yako; ambayo mimi na Watanzania wenzangu tuliaminishwa ilikuwa dhamira yako – angalao kwa wakati ule – niweze kuilinganisha na utekelezaji wake sambamba na matukio mengine yaliyojiri wakati wa mchakato wa uchaguzi na hatimaye ndani ya utawala wako na hivyo kuendelea kuamini ni kwa busara na baraka zako..."
4 Aprili 2007
Waraka wa kwanza wa Mbowe kwa Kikwete
"...Leo, Mheshimiwa Rais, nimeamua kukuandikia waraka huu. Pengine utashangaa kama watakavyoshangaa wananchi wako wengi unaowaongoza. Najua wengine watahoji, iweje nikuandikie kupitia gazetini na isiwe moja kwa moja. Sababu ni rahisi. Kwa kuandika gazetini, nina hakika itakufikia...."
28 Machi 2007
Kikwete, Mugabe lao moja!
"...KUNA msemo usemao kuwa ukitaka kumfahamu mtu mwangalie marafiki zake. Wengine wanasema, ndege wenye manyoya yanayofanana huruka pamoja. Naam, wako wasemao Waarabu wa Pemba hujuana kwa vilemba
..."
21 Machi 2007
Leo ni raia…, kesho ni askari!
"...MAHABUSU wamegoma. Wamekubali kuendelea kusota ndani kufikisha ujumbe. Wamekubali kuteseka ili kuweka akilini mwa viongozi wetu kuwa, kama hawakubali kutoa haki, kuna siku watalazimishwa kutoa haki. Wanahitaji pongezi..."
14 Februari 2007
Nchi imekwama; tayari Kikwete amelemewa
"...Mawazo yangu si msaafu. Ni fikra mbadala ambazo zinakusudia kujenga hoja mjadala.
Ninaamini wako Watanzania wengi wenye uwezo mkubwa sana wa uongozi. Lakini mfumo wetu hauwapi fursa.
Sasa si siri, nchi yetu imekwama. Ni dhahiri Rais Jakaya Kikwete amelemewa. Yeye hataki au pengine hana ujasiri wa kukiri kuwa chama anachokiongoza hakina jibu la umaskini wa Watanzania.
..."
|