Baraza la Wazee wa CHADEMA linaundwa na wazee ambao ni wanachama hai wa CHADEMA.
Muundo
Muundo wa baraza la wazee wa CHADEMA unazingatia muundo wa chama kama yalivyo BAVICHA na BAWACHA.
Yaani ;
Msingi,
Tawi,
Kata,
Wilaya/Jimbo la uchaguzi,
Mkoa,
Jimbo,
Taifa.
Malengo ya Baraza la Wazee
- Kuwa chombo kikuu cha ushauri wa busara na hekima katika kukiwezesha chama kuendeleza na kufikia malengo yake ya kiuchumi, kisiasa na kijamii.
- Kuwa chombo cha ushauri katika ngazi mbalimbali za chama.
- Kuwa chombo cha utatuzi wa migogoro ndani ya chama na baina ya viongozi.
- Kuwa chombo cha kupatanisha na kuunganisha viongozi.
- Kuhamasisha wazee ndani ya jamii kukipenda, kukienzi na kujiunga na CHADEMA.
- Kubuni na mipango na mikakati ya kuhusisha jamii ya wazee ndani ya jamii kukagua, kukagua, kusimika na kuchagua viongozi bora kwenye chaguzi za ndani na nje ya chama.
- Kubuni na kushauri sera bora zitakazowavutia wazee kujiunga na chama.
- Kubuni na kueneza mikakati ya kutumia mila na desturi za jamii ili kudhibiti uenezaji wa VVU na UKIMWI.
- Kuunda kokasi ya wazee itakayo kuwa na jukumu la kushauri viongozi wa chama ngazi ya wilaya mpaka taifa.
- Kuhamasisha jamii ya wazee kuwa mstari wa mbele katika kuhimiza na kuwa mfano wa maadili mema katika jamii.
- Kushiriki harakati mbalimbali za maendeleo kwa kushirikiana na wazee wa vyama vingine ndani na nje ya nchi.
Kauli mbiu
Kauli mbiu ya baraza la Wazee ni:
CHADEMA ................. |
Vema! |
CHADEMA ................. |
Mabadiliko ya kweli, Uhuru wa kweli! |
WAZEE ..................... |
Hazina ya Busara na Hekima! |
|
|