Baraza la wanawake wa CHADEMA linaundwa na wanawake ambao ni wanachama hai wa CHADEMA.
Vijana wa kike wenye umri kati ya miaka 18 na 35 wanaweza kuwa wanachama wa mabaraza yote mawili, BAWACHA na BAVICHA (vijana).
Uanachama
- Mwanamke ataruhusiwa kujiunga na BAWACHA endapo atakuwa mwanachama hai wa CHADEMA.
- Wanachama watapewa kadi maalumu za BAWACHA.
Muundo
Muundo wa BAWACHA una ngazi saba kuanzia ngazi ya msingi mpaka taifa kama ifuatavyo;
Msingi,
Tawi,
Kata,
Wilaya/Jimbo la uchaguzi,
Mkoa,
Jimbo,
Taifa.
Malengo ya BAWACHA
- Kutambua, kusimamia, na kuendeleza na kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika masuala mbalimbali yanayohusu mustakabali wa chama.
- Kusimamia, kulinda na kuendeleza maslahi ya chama.
- Kubuni na kutekeleza mikakati ya kueneza sera za chama kupitia wanawake ndani ya jamii ya ngazi zao.
- Kubuni na kupanga mafunzo ya wanawake kuhusu masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ili kukabiliana na changamoto.
- Kuhamasisha na kuwawezesha wanawake kushiriki katika chaguzi za chama na serikali.
- Kuhamasisha na kuunda timu za kampeni za wagombea wa chama katika chaguzi za serikali.
- Kuanzisha na kuendeleza ukuaji wa vikundi vya sanaa na michezo kwa wanawake.
- Kushirikiana na wanawake wa vyama vingine na jumuiya mbalimbali za kiraia ndani na nje ya nchi.