lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Habari Mpya
»Waraka wa kwanza
b.part
Mabaraza
»Wanawake
»Vijana
»Wazee
b.part
Barua Pepe
jina la mtumiaji:
neno-siri
rt.bt.spc
bt.part2
Muundo

Muundo wa baraza la vijana wa CHADEMA-BAVICHA kwa kiasi kikubwa unakwenda sambamba na muundo wa chama kuanzia ngazi ya msingi mpaka taifa. Muundo huu uko kama ifuatavyo;

      Msingi, Tawi, Kata, Wilaya/Jimbo la uchaguzi, Mkoa, Jimbo, Taifa.


Uanachama

Kutakuwa na wanachama wa aina tatu;

  1. Wanachama Watarajiwa. Hawa wanaitwa CHEMCHEM, Wana umri kati ya miaka 12 mpaka 17. Hawana haki kushiriki michakato ya uchaguzi na maamuzi ya baraza. Watashiriki shughuli za chama na baraza. Watapewa vitambulisho maalumu vya BAVICHA.

  2. Wanachama wa Heshima. Hawa ni wanachama wa CHADEMA wenye mchango maalumu kwa BAVICHA, Ni wanachama wenye umri zaidi ya miaka 35. Watakuwa na vitambulisho maalumu vya BAVICHA, watashiriki shughuli za BAVICHA lakini hawatakuwa na haki ya kushiriki michakato ya uchaguzi na maamuzi ya BAVICHA.

  3. Wanachama wa kawaida. Hawa ndio wanachama mahsusi wa BAVICHA. Ni vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 35. Watakuwa na kadi za BAVICHA, watashiriki shughuli zote za BAVICHA na watakuwa na haki zote za uanachama wa BAVICHA.

Usisubiri jiunge leo! jiunge sasa!


Malengo ya BAVICHA
  1. Kutambua, kusimamia, kuendeleza na kuhamasisha ushiriki wa vijana katika masuala ya siasa
  2. Kubuni na kutekeleza mikakati ya kueneza sera za chama kupitia vijana ndani ya jamii.
  3. Kubuni na kupanga mafunzo ya vijana kuhusu masuala ya kiuchumi na kijamii.
  4. Kuhamasisha vijana kugombea uongozi ndani ya chama na katika chaguzi za serikali.
  5. Kuanzisha na kurutubisha ukuaji wa vikundi vya sanaa na michezo kwa vijana.
  6. Kubuni na kueneza mipango na mikakati ya kudhibiti uenezaji wa magonjwa mbalimbali yanayo athiri vijana matharan UKIMWI.
  7. Kuwa chemchem ya ushauri kwa chama kuhusu masuala yote yanayohusu vijana ndani ya chama.
  8. Kushiriki harakati mbalimbali za vijana ndani na nje ya nchi.
  9. Kushiriki kikamilifu katika timu za kampeni kwa kushirikiana na uongozi wa chama katika kila ngazi husika.


Kauli mbiu ya BAVICHA

Kauli mbiu ya baraza ni Vijana Nguvu ya mabadiliko, na itakuwa ikitanguliwa na kauli mbiu za chama kama ifuatavyo;

CHADEMA .................
Vema!
CHADEMA .................
Mabadiliko ya kweli, Uhuru wa kweli!
VIJANA .....................
Nguvu ya Mabadiliko!
 
 
lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl