lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Ilani ya Chama
»Utangulizi
»Utekelezaji wa ilani
»Tanzania tuitakayo
»Mfumo wa Utawala
»Elimu Bora
»Afya kwa Wote
»Kilimo cha Kisasa
»Uchumi wenye Ajira
»Michezo
b.part
Habari za Uchaguzi
»Jiandae kwa 2010
»Jiandae kwa 2009
»Ilani ya 2005
»Ripoti ya Uchaguzi
»Gharama za 2005
»Matokeo kura Urais
»Matokeo Ubunge
»Matokeo kimkoa
»Kura za Awali
»Kampeni
b.part
Barua Pepe
jina la mtumiaji:
neno-siri
rt.bt.spc
bt.part2

Mfumo wa Utawala Bora

CHADEMA itabadili Mfumo wa Utawala

  1. CHADEMA inaamini kuwa mfumo mbaya wa utawala wa CCM umechangia kwa kiasi kikubwa hali mbaya ya rushwa na ufisadi uliopo nchini. Kadri siku zinavyosonga mbele ndivyo hivyo hali ya rushwa na kukata tamaa kwa wananchi inavyozidi. CCM ikaona ibadili rushwa na kuiita takrima ili kuendeleza ufisadi wao. Viongozi wengi wamekuwa ni wa kuteuliwa na rais na sio wa kuchaguliwa na wananchi. Hali hii imewafanya wananchi wasiwe na imani na viongozi hao kwani badala ya viongozi kuwajibika kwa wananchi, wananchi wamekuwa wakiwajibika kwa viongozi.

  2. CHADEMA itabadili mfumo wa utawala kwa kuhakikisha kuwa viongozi wote wanachaguliwa na wananchi ili wawajibike kwa wananchi. Vyeo vya ukuu wa wilaya na mikoa vitafutwa. Badala yake mabaraza ya kanda na halmashauri za wilaya na manispaa zitasimamia shughuli zote za utendaji. Wananchi kuchagua Meya au Wenyeviti wa Halmashauri. Mikoa itapunguzwa na itaitwa majimbo yatakayokuwa nane. Itaimarisha Serikali ya Kijiji kama chombo cha msingi cha uongozi.


  3. Itahakikisha utawala bora. Itarejesha nyumba za Serikali walizojiuzia viongozi kiupendeleo. Itarejesha Serikalini mali zote zilizohodhiwa na CCM kama viwanja vya mpira, maegesho ya magari na majengo


  4. Itavunja PCB na kufanya rushwa kuwa kosa la jinai chini ya Mkurugenzi wa makosa ya jinai.


  5. Itawezesha wananchi kuandika katiba mpya mapema iwezekanavyo. Madiwani na Wabunge kuwajibishwa na wananchi kwa mujibu wa Katiba.


  6. CHADEMA itaheshimu haki za binadamu: Itawapatia polisi maslahi na mafunzo zaidi ili waweze kusimamia kazi zao kwa haki. Itapiga marufuku VEO na WEO kutishia, kunyanyasa na kunyang'anya mali za wananchi.


  7. CHADEMA itasimamia Muungano unaokubalika. Ili kuhakikisha kuwa pande zote mbili zinanufaika na muungano, patakuwa na mkutano wa Katiba. Mkutano huo utaweka mfumo wa muungano unaokubalika na pande zote.


Serikali ya CHADEMA itaimarisha Uchumi

  1. CHADEMA inaamini kuwa uchumi katika nchi yoyote ile ndio chimbuko la maendeleo. Uchumi unapokuwa duni na nchi inakuwa maskini. Hali kadhalika uchumi unapokuwa mzuri na nchi inakuwa na maendeleo. Hii ni kusema kuwa uchumi ndio kipimo cha maendeleo ya nchi. Inasikitisha sana kuona Tanzania pamoja na utajiri wote ilio nao, bado uchumi wetu uko chini mno. Katika nchi 208 duniani Tanzania ni nchi ya 206 kwa umasikini (World Economic Report: 2004). CHADEMA itaimarisha uchumi kwa kuboresha sekta zote ili ziweze kuliingizia taifa fedha za kigeni kama vile sekta za madini, utalii, kilimo, viwanda n.k.

  2. CHADEMA inaamini kuwa wanawake wamekuwa wakichangia uchumi wa nchi hii kwa kiasi kikubwa. Vilevile historia imethibitisha kuwa mfumo dume katika nchi nyingi za Afrika umekuwa ukiwakandamiza na kuwanyanyasa wanawake katika kila sekta zikiwamo za elimu, ajira na hata zile za ustawi wa jamii. Ni katika mazingira haya basi CHADEMA imeona haja ya kuboresha maisha ya wanawake kwa kuwawezesha waweze kujiletea maendeleo yao. Hii ni pamoja na kuwaendeleza kielimu; kuwapatia mikopo na kuhakikisha kuwa kuna usawa katika ngazi zote za utawala.


  3. CHADEMA itatunga na kutekeleza sera zinazojali watu masikini. Itawezesha Watanzania wanawake kwa wanaume kumiliki uchumi wao wenyewe. Itawezesha kila Mtanzania kumiliki mali bila mizengwe ikiwemo mali za vipaji.


  4. Kodi zinazotozwa zitawekwa wazi. Itapunguza VAT mpaka 16%. Tutaziba mianya ya ukwepaji kodi na kutoa misamaha ya kodi pale tu inapobidi na lazima iidhinishwe na Bunge. Itafuta kodi zote za huduma na bidhaa za akina mama wajawazito na watoto.


  5. Itaongeza ajira. Itatengeneza ajira kuimarisha sekta za ujenzi, madini, kilimo, utalii na huduma za jamii. Itaweka kipaumbele kwa sekta za uchumi zinazotengeneza ajira kwa watu wengi mfano kilimo. Kwa kuwa kipaumbele kimewekwa kwenye elimu, CHADEMA inaamini kuwa shule nyingi zaidi zitajengwa. Kwa hivyo basi waalimu zaidi wataajiriwa. Vilevile, ajira nyingine zitatokana na sekta binafsi. Wananchi wengi hasa vijana watajengewa mazingira mazuri kwa kupewa mikopo kwa ajili ya kuanzisha miradi mbalimbali. Itatoa leseni za bure na likizo ya kodi kwa vijana wafanyabiashara ndogondogo na vijana wanaojishughulisha na uzalishaji mali.
  Kwenye Elimu tutafanya nini?


lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl