|
|
|
|
|
|
Michezo imesahaulika
-
CHADEMA inaamini kuwa michezo ni muhimu sana kwa afya lakini pia inaleta sifa kwa Taifa. Kwa mfano Tanzania
ilifahamika sana mwaka 1976 wakati Filbert Bayi alipotwaa medali ya dhahabu; Klabu ya Simba ilipofikia fainali za klabu bingwa
ya Afrika. CHADEMA tunajiuliza mafanikio hayo yameenda wapi? Kuna tatizo gani?
-
Michezo itawapatia vijana ajira. CHADEMA itawaandaa watoto na vijana wadogo (yoso chini ya miaka 15)
wenye vipaji vya kucheza kandanda na riadha kwa ajili ya kuunda kikosi cha taifa kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitano.
Vijana hawa watapangiwa vituo maalum, mafunzo maalum na chakula maalum. Pia kutakuwapo na chombo cha kandanda ambacho
kitakuwa na mtandao nchi nzima na kushirikisha wanamichezo kuanzia ngazi ya vijiji na kujumuisha taasisi mbalimbali kama
vile shule na makundi mbalimbali ya kijamii.
|
|
 |
 |
|
 |
 |
|