lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Ilani ya Chama
»Utangulizi
»Utekelezaji wa ilani
»Tanzania tuitakayo
»Mfumo wa Utawala
»Elimu Bora
»Afya kwa Wote
»Kilimo cha Kisasa
»Uchumi wenye Ajira
»Michezo
b.part
Habari za Uchaguzi
»Jiandae kwa 2010
»Jiandae kwa 2009
»Ilani ya 2005
»Ripoti ya Uchaguzi
»Gharama za 2005
»Matokeo kura Urais
»Matokeo Ubunge
»Matokeo kimkoa
»Kura za Awali
»Kampeni
b.part
Barua Pepe
jina la mtumiaji:
neno-siri
rt.bt.spc
bt.part2

Hali ya Mkulima wa Tanzania Ikoje?

Hali Halisi ya Elimu Ikoje Tanzania?

  1. Kilimo kimedorora. Licha ya Kilimo kuchangia asilima 44% ya pato la taifa Wananchi bado wanategemea jembe la mkono na mvua zisizotabirika. Barabara hazifiki vijijini na hivyo mazao kuoza kabla ya kufika sokoni.

  2. Soko linalonyonya wakulima. Wachuuzi wanadhulumu wakulima kwa kununua mazao kwa bei ya kutupa. Sera potofu za soko holela zimeua kabisa motisha wa wakulima.


  3. Tunauza mazao ghafi. Hakuna viwanda vidogo vya kuhifadhi na kusindika mazao ya kilimo.


Serikali ya CHADEMA itafanya nini?

  1. CHADEMA inatambua umuhimu wa kilimo katika maisha ya Mtanzania. Asilimia 80 ya Watanzania wanategemea kilimo. Tanzania ilikuwa ni nchi pekee katika Afrika iliyokuwa na kiwango kikubwa cha uzalishaji wa mazao ya chakula katika miaka ya sitini na sabini. Hivi sasa Tanzania inategemea misaada ya vyakula kutoka nje na uigizaji wa vyakula umekuwa ukiongozeka kila siku. Hii ni aibu kwa nchi yetu iliyo na vyanzo vingi vya maji kama vile mito na maziwa. Kilimo cha umwagiliaji hakipo tena. Kwa CHADEMA, sekta ya kilimo itaboreshwa na kilimo cha umwagiliaji kitapewa kipaumbele.

  2. Itafuta kodi. Kodi zote za pembejeo za kilimo ikiwemo VAT zitaondolewa. Itatoa ruzuku kwa wakulima wetu. Itanzisha kilimo kikubwa cha umwagiliaji maji.


  3. Soko la mazao. Soko holela litadhibitiwa. Itaweka kipaumbele kujenga miundo mbinu ya barabara ziendazo vijijini. Itatoa motisha na ushauri kwa wakulima kuzalisha mazao mbadala ya biashara kama maua, viungo na mboga.


  4. Usindikaji. Itatoa ruzuku na motisha kwa uzalishaji wa chakula na usindikaji wa mazao ya kilimo. Itahamasisha wakulima kuuza bidhaa zilizoongezwa thamani.

  Uchumi wa aina gani chini ya uongozi wa CHADEMA?


lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl