lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Ilani ya Chama
»Utangulizi
»Utekelezaji wa ilani
»Tanzania tuitakayo
»Mfumo wa Utawala
»Elimu Bora
»Afya kwa Wote
»Kilimo cha Kisasa
»Uchumi wenye Ajira
»Michezo
b.part
Habari za Uchaguzi
»Jiandae kwa 2010
»Jiandae kwa 2009
»Ilani ya 2005
»Ripoti ya Uchaguzi
»Gharama za 2005
»Matokeo kura Urais
»Matokeo Ubunge
»Matokeo kimkoa
»Kura za Awali
»Kampeni
b.part
Barua Pepe
jina la mtumiaji:
neno-siri
rt.bt.spc
bt.part2

Elimu Bora

Hali Halisi ya Elimu Ikoje Tanzania?

  1. Ubora wa elimu Tanzania umeporomoka. Wanafunzi wanarundikana madarasani na wengine hata kusomea chini ya miti. Mitaala haiendani na hali halisi, vipaji haviendelezwi. Mazingira ya shule hayana mtazamo wa kijinsia na hayawajali watoto wenye ulemavu. Mfumo wa elimu ya msingi haumwandai mwanafunzi kuwa raia wa kujitegemea anapohitimu.


  2. Bajeti ya Elimu finyu. Waalimu ni wachache, wamefukarishwa na hawaendelezwi kitaaluma. Shule na vyuo hazina vifaa vya kuweza kutosheleza ongezeko la wanafunzi.


  3. Gharama za elimu bado ni mzigo mkubwa kwa familia masikini. Wazazi wengi wameshindwa kupeleka watoto wao katika shule za sekondari na vyuo vya elimu ya juu ilhali walionacho wachache wanasomesha watoto wao katika shule za gharama kubwa. Matokeo yake mfumo wa elimu unajenga matabaka ya matajiri walioelimika na maskini mbumbumbu.


Serikali ya CHADEMA itafanya nini?

  1. CHADEMA inaamini kwamba elimu ndio chimbuko la maendeleo ya binadamu yeyote yule. Tunatambua kwamba mataifa yaliyoendelea mengine yakiwa ni machanga kama Tanzania yamezingatia kuwekeza katika elimu. Kwa CHADEMA elimu ndio sekta ongozi katika kuchochea maendeleo, mabadiliko na uhuru wa kweli. Kwa lengo hili basi, CHADEMA itaboresha elimu kwa kuipa kipaumbele.

  2. Itabadili mitaala ya elimu. Mitaala italenga mahitaji na maslahi ya taifa, na kuchochea fikra, udadisi, ugunduzi na kuendeleza vipaji. Masomo ya biashara na kilimo yatarejeshwa katika mitaala. Mashindano ya Umiseta na Umitashumta yatarejeshwa. Elimu ya awali mpaka kidato cha pili itakuwa ya lazima na bure kwa kila Mtanzania.


  3. Bajeti ya elimu kupanda kutoka 18% mpaka 35%. Itajali waalimu kwa kuboresha kipato, makazi na mafunzo yao. Shule na vyuo vitapatiwa vifaa vya kiada na ziada vya kutosha.


  4. Itapunguza mzigo wa gharama za elimu kwa Watanzania maskini. Itatoa ruzuku kwa shule za sekondari na vyuo vya elimu ya juu. Itabadili shule za serikali kuwa ni vituo vya ubora wa elimu ili kuondoa matabaka.
  CHADEMA inasemaje kuhusu Afya?


lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl