lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner


Maelezo ya Hoja ya Kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge


  1. Mheshimiwa Spika,
    Mpaka sasa hakuna maelezo yaliyotolewa kuwa tuhuma zote hizo zilizoibuliwa kwa njia mbalimbali, kama vile vyombo vya habari, taarifa za ndani ya BOT, na kadhalika, kwa kipindi kinachoishia Juni 30, 2006 zimejibiwa. Inawezekana kabisa kuwa hizi ni chache tu za tuhuma zilizojitokeza. Aidha, ripoti ya ukaguzi wa mahesabu ya Benki Kuu haijawasilishwa bungeni rasmi, kinyume na masharti ya lazima ya Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006. Kwa hiyo ni halali kuamini kuwa Benki Kuu lipo tatizo la msingi hadi pale itakapothibitishwa vinginevyo.

  2. Kwa mujibu wa kipengele cha 2.1 cha barua ya waraka wa wakaguzi wa nje cha 21 Decemba, 2006, wakaguzi wa mahesabu hawakupewa kwa ajili ya ukaguzi mkataba kati ya Serikali na Benki Kuu kuhusu ununuzi wa dhamana hizo.

  3. Mhe. Spika, mawasiliano ya kiofisi yaliyothibitishwa na wakaguzi yanaonyesha kuwa, baada ya ununuzi huo wa dhamana, Benki Kuu ilizibadilisha dhamana hizo kwa dola za kimarekani 118,396,460.36 na kuzipeleka kwenye akaunti isiyojulikana ya Nedbank Ltd. ya Afrika Kusini. Benki hiyo ilipozipokea fedha hizo kupitia HSB Bank ya New York, Marekani ikiwa ni malipo ya madeni ya kampuni mufilisi ya Meremeta Ltd. Sehemu nyingine ya fedha hizo zipatazo Dola za kimarekani 13,736,628.73 zililipwa kwa kampuni ya TANGOLD kwenye akaunti ya kampuni hiyo iliyoko Benki ya NBC Corporate Branch iliyoko jijini Dar-Es-Salaam.

  4. Mhe. Spika, tofauti na Bunge hili lilivyoelezwa mara kadhaa, Meremeta Ltd. ni kampuni binafsi ya kigeni iliyoandikishwa tarehe 19 Agosti, 1997 katika kisiwa cha Isle of Man nchini Uingereza na kupewa namba ya usajili 3424504, ikimilikiwa na TRIENNEX (PTY) LTD ya 3rd Floor, West Wing 11 Alice Lane Sandton, South Africa, ikiwa na hisa 50 za kawaida ya GBP 1.0 kila hisa na msajili wa Hazina (Treasury Registrar) wa S.L.P 9111, Madaraka Avenue, Dar-Es-Salaam, naye akiwa na Hisa 50 kila moja GBP 1.0. Kwa upande wa Tanzania, Kampuni ya Meremeta ilipewa Hati ya kutimiza masharti (Certificate of Compliance) yenye na.32755 ya tarehe 3 Oktoba, 1997 . Hata hivyo, Meremeta ilifilisiwa (dissolved) Uingereza tarehe 10/01/2006. Hakuna ushahidi kuwa kwa Tanzania Kampuni hii imefilisiwa au vipi, kwani ‘Taarifa na takwimu muhimu kuhusu Sekta za Nishati na Madini’, ya Julai, 2007, inaonyesha kuwa Meremeta bado inafanya kazi, na inazalisha Tani 2.27 za dhahabu. Kama Serikali inasema Meremeta imefilisiwa na Mali zake kuhamishiwa TANGOLD hali hii inaelezwa vipi? Taarifa hizi za utata zinaashiria nini?

  5. Mhe.Spika, utata pia unaongezeka, kutokana na ushahidi kuwa wenye hisa wengine wa Meremeta kama ilivyoandikishwa Uingereza ni London Law Services Ltd, wa Temple Chambers, Temple Avenue, London, EC4Y,OHP, na London Law Secretarial Ltd wa anuani hiyo hiyo, kila mmoja wao pia akiwa na hisa moja moja. Kwa kuzingatia kuwa Hati zilizowasilishwa kwa Msajili wa Makampuni Tanzania zinaonyesha kuwa Msajili wa Hazina anamiliki Hisa 50 na Triennex (PTY) nayo ina hisa 50, hizi hisa mbili za London Law Services Ltd, na London Law Secretarial ltd zinaelezwaje?

  6. Mhe.Spika, uhusiano kati ya Kampuni inayoshughulikia dhahabu na Kampuni ya Sheria, mathalan ya ‘Secretarial’ inaongezea mashaka makubwa zaidi. Mhe. Spika kuna fumbo kubwa hapa linalohitaji kufumbuliwa. Isitoshe, wakati Meremeta inasajiliwa Tanzania waliwasilisha, na ninanukuu barua ya Brela “..two uncertified photocopies of share certificates issued by the company..”. Ni kwa nini Kampuni inayomilikiwa na Serikali inawasilisha Taarifa yenye utata kinyume na taratibu za Sheria? Taarifa iliyoko kwa msajili wa Makampuni Uingereza inaonyesha kuwa, ‘Meremeta haina matawi” (There are no branches associated with this company) na ‘ There are no overseas details associated with this company’.

  7. Mhe. Spika, Taarifa hizi zinaleta hisia za mashaka, udanganyifu, ghiliba na kujenga wasiwasi kuwa kuna jambo si sahihi. Huenda ndiyo maana Serikali hata baada ya kuhojiwa ndani ya Bunge hili imeendelea kutoa majibu yenye kukinzana. Hoja ya msingi ni kwanini Meremeta ambayo kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Serikali ndani ya Bunge, kuwa ni kampuni iliyoanzishwa kwa lengo la kusaidia Jeshi letu la Wananchi (Kikosi cha Nyumbu) imeandikishwa nchi ya kigeni? Kwanini Taarifa hata ya matawi au ofisi yake iliyoko Tanzania haiko kwa msajili Uingereza. Usiri huu mkubwa unaashiria nini? Kampuni hii iliyojaa usiri mkubwa, ndiyo iliyolipwa mabilioni ya Fedha za walipa kodi wa Tanzania. Bunge lako Tukufu, Mhe. Spika, lina wajibu kwa niaba ya Wananchi kufumbua utata huu kwa njia ya uchunguzi wa kina unaoweza kufanywa tu na Kamati Teule ya Bunge.

Mheshimiwa Spika,
kumbukumbu zinaonyesha kuwa uhamisho wa fedha uliotajwa hapo juu yaani Dola za Marekani 131,736,628.73 sawa na Shillingi Bilioni 155 ulifanywa kufuatia maelekezo (directive) yaliyokuwa yametolewa kupitia nyaraka Kumb. Na EB/AG/4001162 ya tarehe 20 Desemba, 2005, waraka na.EB/AG/40/01/162 ya tarehe 27 Desemba, 2005, na waraka na. EB/AG/40/01/163 ya tarehe 27 Desemba, 2005 zilizoelekeza uhamisho wa fedha hizo ambazo baadaye ndizo zilizobadilishwa kuwa Dola za marekani kama tulivyoeleza hapa juu. Ufumbuzi wa msingi wa maelekezo haya nao unahitaji kuchunguzwa kwa kina na Kamati Teule ya Bunge.

Mheshimiwa Spika,
Lengo la kuunda Kamati Teule ya Bunge lako Tukufu ni kuchunguza tuhuma na utata huu ili kupata majibu ambayo si rahisi kuyapata bila uchunguzi wa kina na chombo huru, chombo kisicho cha Serikali, ili kubaini ukweli kufanyika au vinginevyo wa tuhuma zilizopo. Na hasa kubaini, kwa nini ililazimu fedha za walipa kodi zitumike kulipia madeni ya Kampuni ya Meremeta Ltd ambayo ni kampuni binafsi na/au ya kigeni iliyosajiliwa nje ya nchi. Kwa mujibu wa taratibu za Sheria ya Makampuni, hata kama kampuni hiyo ingekuwa ni mali ya Serikali kwa asilimia mia moja, ingebidi wadai wake kama vile Nedbank, wapeleke madai yao kwa mfilisi wa kampuni hiyo kama wadai wengine. Jambo hili linatia mashaka na linahitaji lipate majibu ya kina kuondoa mashaka yotote yale yenye kuzaa hisia ya uwepo wa ufisadi na ubadhirifu mkubwa ndani ya BOT.

 

rudi...     inaendelea...

 

lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl