lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner


Maelezo ya Hoja ya Kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge


  1. Kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania, ya mwaka 2006,Kifungu cha 21 Taarifa ya Ukaguzi ya Benki Kuu inatakiwa iwe imewasilishwa Bungeni ndani ya miezi sita tangu mwisho wa mwaka wa Fedha husika. Hadi leo ninapowasilisha Hoja hii, yaani zaidi ya mwaka mmoja tangu tarehe Hesabu za mwisho zilipotakiwa kufungwa, taarifa ya ukaguzi haijawasilishwa Bungeni, jambo linalotia utata na mashaka makubwa, hasa ikiwianishwa na taarifa zilizoko za tuhuma ya ubadhirifu mkubwa ndani ya BOT.

  2. Mhe. Spika, taarifa rasmi tuliyonayo ni kuwa Ukaguzi huu umechelewa sana baada ya aliyekuwa Mkaguzi wa Mahesabu ya BOT yaani kampuni ya kimataifa ya Deloitte and Touche ya Afrika ya Kusini ambao ndio pia waliokagua mahesabu ya mwaka 2004/2005- iliyotolewa 14th Octoba, 2005, ( kwa kushirikiana na Kampuni ya TAC Associates) ilisimamishwa katika mazingira ya kutatanisha. Baadhi ya mambo ya msingi aliyoyayahoji Mkaguzi huyo ni pamoja na suala la “Interest Free loan Provided to Government’’ kiasi cha Tshs Bilioni 69 zilizotolewa katika sura ya EPA (External Payment Arrears), ‘’Security for Investment in Mwananchi Gold Company Ltd’ ambapo mkopo wa dola za Marekani 2,609,478.55 hazikuwa na mdhamana “security” ( kama imewekwa sasa Kamati Teule ni lazima ichunguze hiyo ‘security’ imewekwa tarehe ngapi na kwa nini kwa muda wote huo haikuwepo na ni kitu gani kimewekwa kama ‘Security’), pamoja na ‘Payment for Legal Fees’. Mambo haya yote yameendelea kuwa hivyo hadi taarifa ya ukaguzi ya 21 Desemba, 2006 jambo ambalo au linatia mashaka makubwa ya ubadhirifu, au uzembe katika ‘management’ ya Mali za Taifa zinazosimamiwa na BOT. Mkaguzi wa Deloitte and Touche wakati anasimamishwa anasemekana alikwisha kufika mbali katika kazi ya ukaguzi. Sababu zilizotolewa na BOT zinatia mashaka, kwa vile kwa mujibu wa Sheria iliyounda ofisi ya CAG inampa CAG mamlaka ya kuteua kampuni yeyote ya ndani au ya nje, kufanya ukaguzi kwa niaba yake, kama anavyotaka kufanya sasa katika kinachoitwa ‘Special Audit’. Mazingira haya yaliyofanya Mkaguzi huyo wa kimataifa kusimamishwa ghafla baada ya kuibua hoja nzito, nayo yanahitaji kuchunguzwa kwa kina kama hayana sura ya kuficha jambo au vinginevyo.

  3. Hata hivyo, taarifa mbalimbali za ndani ya BOT, zinaonyesha kuwa Benki Kuu kwa kipindi kilichoishia tarehe 30 Juni 2006 kuna maeneo mathalan manane yenye utata yanayoonyesha ubadhirifu na uvunjaji wa sheria za nchi katika uendeshaji wa Benki Kuu ya Tanzania. Vipengele hivyo ni kama ifuatavyo:

  • Benki Kuu kununua kutoka Serikalini dhamana maalumu za hazina zinazoiva katika kipindi cha miaka mitano zenye thamani ya shilingi bilioni 155 na kuzihamishia katika akaunti isiyojulikana na kwa matumizi yasiyojulikana;

  • utosajili dhamana za mikopo iliyotolewa na Benki Kuu kwa Kampuni binafsi ya Mwananchi Gold Company kufuatana na matakwa ya sheria za nchi, jambo ambalo linabatilisha dhamana za mikopo hiyo kisheria;

  • Majina ya wadai walioingiza fedha za kigeni na kiasi cha fedha wanachodai baada ya fedha zao kubadilishwa kuwa fedha za Tanzania kutowasilishwa kwa wakaguzi hadi 21 Decemba, 2006 hivyo usahihi wa malipo ya jumla ya shilingi bilioni 131,950,750,000 kutokupatikana, na hata baada ya tarehe hiyo hakuna ushahidi wa wazi ulioweza kuthibitishwa.

  • Kuwepo kwa mashaka kuhusu mikataba ya ujenzi wa majengo ya makao makuu ya Benki Kuu barabara ya 10 Mirambo, Dar es salaam na Gulioni, Zanzibar uliogharimu jumla ya shilingi bilioni 522,459,255,000 bila majengo hayo kukamilika hadi sasa. Kutokana na kasoro hii taarifa za ndani ya BOT zinaonyesha utata wa kuoanisha thamani halisi ya majengo hayo kulingana na masharti ya kazi yaliyowekwa na mikataba, kazi iliyofanyika na thamani halisi ya miradi hiyo na mabadiliko (variation) ya mara nyingi ya gharama bila kuonyesha mamlaka halisi iliyoidhinisha mabadiliko hayo;

  • Benki Kuu kulipa malipo makubwa kwa wataalamu kupita kiasi, hii ikiwa ni malipo yaliyofanywa kwa wanasheria na pia malipo yaliyofanywa kwa wahasibu wa miradi ya madini ya dhahabu;

  • Mdhamana wa miaka 5 kwa niaba ya Serikali wa zaidi ya Shillingi Bilioni 36 kwa makampuni 4 yanayouza Maua na mboga mboga nje nchi. Hadi tarehe 21 Decemba, 2006 hapakuwa na ‘Security’ yeyote iliyotolewa na Makampuni hayo kama inavyotakiwa na sheria na wala hapakuwa na muda maalum ambapo fedha hizo zilitakiwa kulipwa.

  • Hivi karibuni kama ilivyoripotiwa na vyombo vya Habari, kuwa“BOT in more trouble over 72bn Loan guarantee as Kagera Sugar Lenders want their money back”, This Day, ISSN 1821-5262 na 435 la Jumanne, 17 Julai, 2007, na wala Serikali wala BOT havikukanusha au kutoa tamko lolote kuhusu jambo hili. Kwa mujibu wa taarifa hiyo kumetokea mgogoro wa mdhamana huo wa shillingi Bilioni 72 uliotolewa kwa Kampuni binafsi ya kibiashara ya Sukari ya Kagera. Inaelezwa kuwa BOT inaweza kuwajibika kulipa deni pamoja na Riba inayozidi billioni 50. Fedha zinazolipa BOT zinatokana na kodi za wananchi na mapato mengine ya Taifa. Fedha hizi ni nyingi sana kulipwa kwa kodi ya mwananchi mlalahoi na zingeliweza kufanya kazi nyingi za maana zaidi. Kushindikana kulipwa kwa mkopo huo maana yake ni Benki Kuu kutakiwa kulipia mikopo hiyo na riba.

  • Kutokuwepo kwa utawala bora na uadilifu ndani ya Benki Kuu na/au miongoni mwa watendaji wake wakuu. Hali ilivyo hivi sasa kwenye Benki Kuu ya Tanzania, Gavana wa Benki hiyo pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi wa Mahesabu ya Benki Kuu. Kofia hizi mbili zimeinyima Benki Kuu uwezo wa kuhoji na/au kusimamia matumizi ya fedha za Benki Kuu. Pia kitendo cha Gavana wa Benki Kuu kuwa mkurugenzi katika makampuni binafsi aliyoyapatia mikopo kinaonyesha mgongano wa maslahi na ufisadi katika uendeshaji wa Benki Kuu; na

  • Benki Kuu kujitwika wajibu ambao sio wake kisheria wa kuingia kwenye biashara ya fedha kama benki za kawaida kwa kukopesha makampuni binafsi.

 

rudi...     inaendelea...

 

lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl