|
|
|
|
|
|
|
Hotuba ya Kiongozi wa Upinzani na Waziri Kivuli wa Fedha
Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed (MB)
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2007/2008
I. UTANGULIZI
- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Kambi ya Upinzani naomba upokee shukrani zetu za dhati kwa kunipa nafasi hii ili nitoe maoni ya Kambi ya Upinzani kuhusu hotuba ya bajeti ya mwaka wa fedha 2007/2008 kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Kifungu cha 43(5)(b)(c) na 81(1) toleo la Mwaka 2004.
- Mhe. Spika, Awali ya yote naomba kutoa shukurani zangu za dhati kwa wabunge wote wa Kambi ya Upinzani kwa ushirikiano wao mkubwa walionipa hadi kuniwezesha kusimama mbele yenu kuwasilisha hotuba ya maoni ya Kambi ya Upinzani, kutokana hoja iliowasilishwa na Waziri wa fedha tarehe 14.06.07. Mhe. Spika, Wabunge wa Upinzani na wabunge wote kwa jumla wao, kwa pamoja tuna wajibu wa kushirikiana katika kuwatumikia Watanzania kwa lengo kuu la kuwaondolea Umasikini uliokithiri, Maradhi na Ujinga pamoja na kujenga UTAIFA wetu wa dhati. Mwenyezi Mungu aziweke pamoja nia zetu na kuzibariki katika kutekeleza azma hiyo.
- Aidha Mhe. Spika naomba niwashukuru wapiga kura wa Jimbo langu la Wawi kwa kuendelea kuniunga mkono katika kazi walizonikabidhi katika kipindi cha 2005-2010. Nawaahidi, kuwa kwa uwezo wa Mwenyeezi Mungu nitawatumikia kwa uadilifu mkubwa.
- Mhe. Spika, mnamo tarehe 14.06.2006 Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete alifanya mazungumzo na wabunge wa CCM na hatimaye wabunge wa Kambi ya Upinzani. Katika kikao hicho pamoja na mambo mengine mengi, Rais aliendelea kutoa ahadi yake ya kuumaliza mpasuko wa kisiasa ulioko Zanzibar na kusema “Tumeisha anza, siyo rahisi sana lakini tutaumaliza.”
- Mhe. Spika, Kambi ya Upinzani itaendelea kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais katika kuutafutia ufumbuzi mpasuko wa kisiasa wa Zanzibar pamoja na kero za Muungano, ila Kambi ya Upinzani ingelipenda kuweka bayana kwamba imani ya Watanzania inaendelea kupungua siku hadi siku kutokana na ahadi kama hizo kutolewa na Rais aliyemtangulia na pia kutokutekelezwa kikamilifu kwa miafaka ya 1999 na 2001 kati ya CCM na CUF .
- Mhe. Spika, kwa kuwa Mhe. Rais mwenyewe ameahidi kutembea kwenye maneno yake, sisi Kambi ya Upinzani tunapongeza hatua iliochukuliwa ya kuanza mazungumzo ya kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa mpasuko wa kisiasa Zanzibar,ila tunawaomba wale walioko kwenye mazungumzo hayo waelewe kuwa muda umekuwa mrefu, ni vyema Watanzania wakajulishwa hatua iliyofikiwa ili kuondoa shaka juu ya mazungumzo yanayoendelea.Watanzania walio wengi wanapenda kuwa na imani na kauli ya Rais, na Sisi katika Kambi ya Upinzani tunaahidi kuzidi kufuatilia kwa karibu mwenendo mzima wa mazungumzo huku tukielewa kuwa muda wa subira nao unazidi kuyoyoma. Mheshimiwa Spika, naomba kwa niaba ya Kambi ya Upinzani,kukushukuru wewe,naibu wako na watendaji wa ofisi yako,wakiongozwa na Katibu wa Bunge,kwa kutupatia fursa mbali mbali sisi wabunge kujifunza shughuli za mabunge ya wenzetu.Moja tulilojifunza katika mabunge mengi,kambi ya upinzani huwa inapata fursa ya kutoa bajeti mbadala,kwa kwetu hili bado ni geni na hata kanuni zetu zina mapungufu,hata hivyo kwa idhini yako tutaendelea na utaratibu wa kutoa maoni kama kawaida ila tu, mara hii tumezama kwa undani zaidi ili kutoa ushauri na suluhisho kwa mtazamo wetu.Kutokana na muda na uzoefu mdogo tulionao,tunaomba radhi kama kuna mapungufu katika kutoa ushauri wetu,uwe wa kimaandishi au kitakwimu. Nia yetu ni kumsaidia Mtanzania aondokane na umasikini wa kila aina.
- Mhe. Spika, naomba kumpongeza Mheshimiwa Waziri wa Fedha Mhe. Zakhia Hamdan Meghji (Mb), Manaibu Waziri, Katibu Mkuu na Manaibu wake, pamoja na wakuu wa vitengo na asasi zilizochini yao kwa kazi nzito ya maandalizi ya Bajeti hii pamoja na kwamba Kambi ya upinzani ina maoni tofauti katika baadhi ya maeneo ya wigo wa mapato ya ndani, kodi katika mafuta, na viwango vya mishahara ya wafanyakazi wa chini na mapato yatokanayo na raslimali zetu.Tofauti hizo nitazielezea baadaye.
- Mhe. Spika, naomba nitumie fursa hii fupi kuwakumbusha Watanzania kupitia Bunge lako Tukufu, kuwa tokea Nchi yetu ipate Uhuru (Tanganyika) 1961 kukawa na “Republic of Tanganyika” na baada ya Mapinduzi (Zanzibar) 1964, kukawa na “People’s Republic of Zanzibar” na hatimaye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Nchi yetu imeongozwa na TANU na ASP na Hatimaye CCM. Hivyo ni dhahiri kuwa mafanikio na mapungufu yote ya maendeleo ya Nchi yetu yametokana na Uongozi na Sera za CCM, ambayo ni mrithi wa TANU Na ASP.
- Mhe. Spika ni wajibu wetu sote kujiuliza, katika kipindi hichi chote cha uongozi wa aina moja. Je kwa sera zilizokuwepo Mtanzania wa kawaida maisha yake yameboreka? Kwamba sasa anaweza akapata angalau milo miwili bila ya wasi wasi? Mwananchi wa kawaida anaweza akasomesha watoto wake na watoto hao wakasoma vizuri na hatimaye wakapata ajira? Au anaweza kujiajiri kwa kupata mikopo kwa urahisi yenye riba nafuu? Au Anaweza kupata huduma ya kijamii bila ya kulipia kwa gharama kubwa na kama anaweza kupata bei muafaka ya mazao yake kwa kuuza anakotaka kama ilivyokuwa kabla ya Uhuru na Mapinduzi? Je hata anayefanya kazi amepata mshahara unaokidhi muda wake wa kazi na mahitaji yake? Mheshimiwa Spika, tunapo kumbushana haya hatusemi kwamba Tanzania hakuna maendeleo au mabadiliko, lakini je maendeleo hayo ni endelevu kiasi cha kumhakikishia Mtanzania kwamba baada ya “Sera ya Kilimo ni Uhai” ya Mwaka 1976, je tunajitosheleza kwa chakula cha kutosha na hata ukame ukitokea tuna chakula cha akiba? Au bado tunaendelea kuhemea chakula? Kwamba tuliwahi kuwa na hekta 450,000 za umwagiliaji sasa zipo 278,888 tu, hayo ni maendeleo endelevu? Kwamba Mwalimu alituambia “ kupanga ni kuchagua” Je , kununua ndege kwapesa taslim Tsh 42 billion, inayoweza kutua katika viwanja visivyozidi vitano katika nchi nzima na hata kushindwa kutua Dodoma ambayo ni Makao Makuu ya nchi na ya Bunge; ndege inayotumia wastani wa Tsh.6 million kwa saa ya kuruka na kuacha kuwatengenezea barabara wanachi wa Kusini ambao ni wazalishaji wakubwa wa Korosho, Muhogo, Ufuta na raslimali za Misitu na au kuacha kujenga zahanati, shule zenye kuwanufaisha wananchi walio wengi bila ya wao kujitolea, ni matumizi mazuri ya raslimali chache tulizo nazo? Au ndio ule msemo wa kiswahili kwamba “Punda afe lakini mzigo wa bwana ufike”.Kwamba huku unataka kumuondolea umasikini, upande wa pili unamuongezea kodi kwa mlango wa nyuma. Kodi ya mafuta ambayo kupanda kwake katika soko la dunia hakutabiriki, ikipanda gharama za uzalishaji nazo zinaongezeka, hivyo mlaji kubeba mzigo wa kodi.Je kwa sera hizi zisizomjali mwananchi, uchumi utakua na umasikini kupungua?
- Mheshimiwa Spika, Bajeti ya mwaka 2007/2008 ni Bajeti ya pili ya serikali ya awamu ya Nne. Lengo letu kama Kambi ya Upinzani ni kupitia utekelezaji wa Bajeti ya mwaka unaokwisha kwa shabaha ya kuonesha mafanikio na mapungufu na kisha kupendekeza njia mwafaka ya kuwa na Bajeti bora itakayoleta nafuu ya maisha kwa wananchi wetu.
- Mheshimiwa Spika, Bajeti ya Serikali ni zaidi ya urari wa mapato na matumizi ya Serikali. Bajeti ni tamko la kisera lenye lengo mahususi katika kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi na kupunguza umasikini miongoni mwa wananchi.Kambi ya upinzani Bungeni chini ya uongozi wangu na msaidizi wangu Mhe. Dr.Slaa,(Mb) Mbunge wa Karatu , inaundwa na vyama vya CUF, CHADEMA, TLP na UDP.Naomba kutumia fursa hii kuvishukuru vyama vyetu kwa kuanza kujenga maelewano ambayo sio tu kusaidia juhudi za kambi yetu kutoa maoni ya pamoja juu ya hutuba ya bajeti ya Waziri wa Fedha bali kuisaidia Serikaali katika muona wa pili wa shilingi.
- Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu tathmini ya Kambi ya Upinzani kwa ufupi utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya mwaka 2006/2007, na baadaye nieleze misingi na shabaha ambayo kama Serikali ingalizingatia Mapato na Matumizi ya Serikali ya mwaka 2007/2008 yangaliboreka zaidi.
II. UTEKELEZAJI WA BAJETI ILIYOPITA
- Mheshimiwa Spika, Katika Bajeti ya mwaka 2006/2007 Serikali ilipanga kutumia jumla ya Tshs. 4.85tr. Kati ya hizo jumla ya Tshs. 2.83tr zilipangwa kutumika kulipia mishahara na matumizi mengine, Tshs. 287.8bn kwa ajili ya Riba, Madeni na mengineyo (mfuko mkuu) na Tshs. 1.7tr kwa miradi ya maendeleo. Katika fedha hizi za maendelo fedha za ndani zilikuwa ni Tshs. 641.7bn tu ambayo ni sawa na asilimia 37 ya Bajeti yote ya maendeleo na hivyo kuifanya Bajeti ya Serikali kuwa tegemezi kwa asilimia 63%.
MFUMO WA BAJETI
-
Mheshimiwa Spika, mfumo wetu wa bajeti bado hauko wazi kiasi cha Wabunge kushindwa kufuatilia kwa undani vifungu vya mapato na matumizi. Wakati Waziri akiwasilisha mtazamo wa bajeti kwenye Kamati ya Fedha na Uchumi, tatizo hili lilijitokeza.Hatuwezi kufuatilia na kujua fungu linaloitwa ‘O/C’ na ‘Employment Allowance’ lina vifungu vingapi vidogo vidogo. Aidha baadhi ya Wizara kama Elimu, Kilimo na Afya, fedha zao zinatoka katika mikondo zaidi ya minne, hivyo wahasibu, hasa wa Halmashauri wanashindwa kufuatilia kwa undani fedha zinazoingizwa katika Halmashauri zao. Utaratibu huu unasababisha kujirudia (double accounting) kwa mapato na matumizi. Kambi ya upinzani inaona haya ni mapungufu makubwa. Mhe. Spika, Hapa kwetu mafungu ya Bajeti yanachukuliwa kwa ujumla jumla tu, hivyo kuwafanya Wabunge kutokufahamu kwa kina matumizi ya mafungu hayo. Hii ni tofauti na nchi nyingine nyingi kama Zambia na Mauritius,Uganda na India kutaja chache tu, zinazofuata mfumo kama wa kwetu wa CPA ambapo hata Mshahara wa Rais unaonyeshwa, Ziara za Rais, kwa mwaka zinajulikana. Aidha ziara zote za Mawaziri, Wabunge na Watumishi wote zinaorodheshwa na hivyo kuifanya kazi ya Wabunge ya kuisimamia Serikali kuwa rahisi lakini pia kuondoa mianya yote ya matumizi hewa.
Kambi ya upinzani inaona haya ni mapungufu makubwa yanayohitaji kurekebishwa mara mmoja, kwani, uwezekano wa kuwa na matumizi mabya na au ubadhirifu/uwizi wa mapato ni mkubwa.
- Mhe.Spika, bado serikali inakusudia kutumia zaidi katika matumizi ya kwaida (tshs.3.886 bl.) kuliko matumizi ya maendeleo (tshs.2,201bn.).Hii ni kama tulivyo wahi kusema kuwa ukubwa wa Serikali utasababisha matumizi makubwa ya kawaida. Kambi ya Upinzani inaona kuna kasoro kubwa ya kiuwiano kati ya matumizi ya kawaida na yale ya maendeleo, hivyo kuchelewesha ukuaji wa uchumi na kupunguza umasikini. Fedha nyingi zinatumika katika uendeshaji wa Serikali kuliko katika maendeleo na huduma za jamii na hivyo kupnda kwa pato la Taifa kutokuwa na manufaa ya moja kwa moja kwa mwananchi wa kawaida.
- Mhe. Spika, Kutokana na taarifa ya Makaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG) katika Wizara na Idara tano tulizochambua, tumebaini kuna upungufu wa makusanyo wa mapato yasiyopungua shilingi 73.8 billion,(Ferry Kivukoni 442.5 million, Veta,762 Millioni; Tansort,71.billon+1.3billion 72.3bn) Aidha,misamaha ya Kodi nayo imekuwa ya kutisha, kwani hadi kufikia mwezi huu wa Juni,inakisiwa Tshs.673 billion zitakuwa zimesamehewa kama kodi. Hiki ni kiasi kikubwa kwa nchi inayoomba misaada kila kukicha. Kambi ya upinzani inaona huu ni upungufu mkubwa wa mapato ya wanyonge wa Watanzania kwa kuyatupa bila utaratibu wa wazi na unaoeleweka.
- Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani, inaomba kumalizia tathmini yake kwa kuomba tena ufafanuzi kutoka kwa Waziri,baada ya wajumbe wake kukosa maelezo katika Kamati Ya Fedha na Uchumi kuhusu mambo yafuatayo:-
- Waziri alieleze Bunge lako Tukufu thamani halisi ya gharama za ujenzi wa majengo ya Benki Kuu ambayo kwa taarifa tuliyo nayo sisi ni kwamba majengo hayo (Twin Towers) yamegharimu si chini ya ya Usd 340million kwa kujenga katika eneo la 40,000 sq.m. wastani wa kila Sq.mita moja imegharimu zaidi ya Dola za Marekani 8000 wakati kwa mujibu wa gharama za ujenzi hapa Tanzania haziwezi kuzidi Usd 800. Kwa bei hii kuna zaidi ya Usd.7200. Miji ambayo ujenzi ni ghali kama New York, London, Tokyo gharama ya majengo kama hayo si zaidi ya Dola za Marekani 2,000 kwa kila kitu ikiwa ni pamoja na gharama ya ardhi, na nakishi mbalimbali . Serikali inasema nini juu ya matumizi haya makubwa ambayo yamefanya ujenzi huo ghali mara nne zaidi ya miji hiyo mikubwa duniani? Serikali inalieleza nini Bunge hili kuhusu taarifa zilizoko kuwa hata tenda ilitolewa kwa utaratibu unaotia mashaka?
- Bunge lililopita tuliomba Bunge lako Tukufu lipewe maelezo juu ya uwekezaji wa BOT katika Mwananchi Gold Mine, kwamba je BOT iliendelea kuwekeza katika kampuni hiyo binafsi na iliwekeza kiasi gani na mapato yaliopatikana hadi sasa ni kiasi gani.Tunaomba Serikali itupatie maelezo ya kina ambayo tuna tumaini yatakuwa tofauti na ya mwaka jana, yatakuwa si majibu ya kisiasa.
- Katika kikao cha bajeti cha 2006/07 Bunge lilielezwa kuwa ule Mradi ulioasisiwa na Marehemu Baba wa Taifa wa kuwapatia wanajeshi wetu fedha kwa ajili ya kuendeshea mradi wa Nyumbu,Meremeta Gold Co. ambayo ilikuwa chini ya uongozi wa Time Mining ya South Africa(baada ya kuichukua kutoka kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania), na kudhaminiwa na BOT kwa USD100million, iko katika hatari ya kufilisika, lakini tukaambiwa kuwa BOT ilikuwa ikifanya tathmini.. Kambi ya Upinzani inapenda kupata taarifa ya kina kuhusu tathmini iliofanywa na BOT ya mradi huo .
- Katika Kamati ya Fedha na Uchumi tuliomba kupewa taarifa juu ya malipo hewa yaliyofanywa na BOT, katika Akaunti ya kulipia Madeni ya Nje (Debt Service Account). Kambi ya Upinzani ina taarifa kuwa si chini ya Dolla za Kimarekani 200 Million zime haulishwa kwa njia hii, kiasi cha kuifanya hata shilingi yetu itetereke kinyume na taarifa tunazopewa za kupungua kwa mauzo ya nje. Pia tulisoma katika vyombo vya habari kuwa IMF na Waziri wa Fedha waliagiza uchunguzi ufanywe,Serikai inasemaje juu uchunguzi wa taarifa hii? Je Serikali inaeleza nini kuhusu utaratibu huu wa Taarifa kutokutolewa kwa Bunge ambalo ni chombo cha Wananchi na Badala yake uchunguzi unaagizwa na Chombo cha Nje yaani IMF? Serikali inaeleza nini kuhusu majukumu ya Bunge hili hasa katika kusimamia rasilimali za nchi hii na jasho la Wananchi?
- Katika Kamati tuliomba kupewa taarifa juu ya JFC, Waziri katika majibu yake kwa kamati(uk2.) alijibu “wakati uamuzi kuhusu mapendekezo ya Tume unasubiriwa,bajeti ya 2007/08 imetenga mgao wa Zanzibar kwa utaratibu wa asilimia 4.5 ya misaada ya kibajeti” Katika hotuba ya Waziri Bungeni uk.47,juu ya mgao huo anasema”Kwa hiyo....... 2007/08 imetenga..........asilimia 4.5 ya misaada ya nje ya bajeti” tunaomba atupe tafsiri sahihi ya kauli zake hizi.
-
Mhe. Spika, wakati tukiwasilisha maoni ya Kambi ya Upinzani katika Bajeti ya 2004/2005 tuliulizia juu ya kukiukwa kwa utaratibu wa kumpata mzabuni wa kuchunguza mauzo ya dhahabu unaofanywa na kampuni ya Alex Stuart Asseyers, mwaka huu tulitegemea Serikali ingelisema ni kiasi gani cha mapato kimepatikana kutokana na taarifa ya Alex Stuwart Asseyers baada ya Serikali kuilipa kampuni hiyo si chini ya USD65,000.000 sawa na Ths. Billion 85 inayotokana na mapato ya mrahaba wa 1.9% kati ya 3% inayopta Serikali kiasi ambacho kingeweza kukopesha wanafunzi 20,000 wa Vyuo Vikuu ambao leo tunawataka walipe asilimia 40% na kutokana na umasikini ulio kithiri hivi sasa vijana wasiopungua mia tatu wanaosomea UALIMU SAUT wamerudishwa makwao kwa kukosa asilimia 40% wakati raslimali zao zinatolewa “sadaka.”
Mhe. Spika, Kambi ya Upinzani na Watanzania kwa ujumla tunaona haya ni mapungufu makubwa katika matumizi ya rasilimali na zaidi pale Serikali inaposhindwa kueleza Bunge lako Tukufu mapato yaliyopatikana kutokana na kazi ya Alex Stuwart Asseyers.
- Mhe. Spika, Japo kuwa kila mwaka kelele zinapigwa kuhusu misamaha ya kodi, bado hali haijawa nzuri. Zaidi ya Tshs.673billion ya mapato yametolewa kama misamaha. Ni lazima tuandae utaratibu kwa mwaka huu kupunguza angalau asilimia 50% ya misamaha hiyo ili kupunguza Rushwa na bajeti tegemezi, lakini pia kuwa na utaratibu ulio wazi zaidi wa kutoa misamaha.
- Mhe. Spika, Katika Hotuba ya Waziri (uk.59) Serikali inakusudia kuanzisha utaratibu wa kupitisha moja kwa moja (fast tracking) bila ukaguzi bidhaa zote zinazoagizwa………Mhe. Spika, utaratibu huu ni mzuri kama upo uadilifu wa kutosha wa walipa kodi na wakusanyaji wa kodi.Mhe.Spika,Serikali ilipoona kuna udhaifu katika utekelezaji Bandarini hivyo wakaamua kukodisha kwa makampuni mbali mbali. Kambi ya Upinzani ingetegemea Serikali kuja na tathmini yautekelezaji wa makampuni hayo ili iwe rahisi kwa Bunge kuamua,juu ya utaratibu unaopendekezawa na Serikali kama usimamiwe na TRA au kampuni binafsi,kwani pia yapo mashaka kwamba kushindwa kwa makampuni yaliyoko bandarini kufanya kazi zao kama inavyotakiwa, itumike njia hii ili wapate wasaa wa kuficha udhaifu wao. Aidha,utaratibu huu unaweza kuwa njia moja ya kuipunguzia mapato Serikali. Kambi ya Upinzani, pamoja na kwamba inakasirishwa sana na kitendo cha wafanyabishara kunyanyaswa wakati wa kutoa mizigo yao, bado haijashawishika na utaratibu huu, hadi hapo Serikali itakapo fanya tathmini ya utekelezaji kwa makampuni yanayofanya kazi kwa niaba ya THA na TRA ili kama ni sifa au lawama ziwe kwa chombo chetu tu.
- Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani, haikubaliani kabisa na ongezeko la kodi katika mafuta ya aina yeyote ile, kwani inapingana na dhana nzima ya kukua kwa uchumi na kupunguza umasikini, inaathiri programu nzima ya Mkukuta na uzalishaji, inamkandamiza mwananchi wa kawaida ikizingatiwa hasa kuwa asilimia 90 ya Watanzania wanatumia mafuta ya Taa kwa matumizi yao ya kila siku. Kambi ya Upinzani itatoa mapendekezo yake juu ya njia bora ya kupata Mapato mengine bila ya kupandisha kodi ya mafuta.
III. MAONI YA KMBI YA UPINZANI JUU YA MFUMO WA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2007/2008
- Mhe. Spika, kwa uchambuzi wetu, mfumo mzima wa Bajeti una mapungufu makubwa. Kwanza hauwashirikishi Wabunge katika maandalizi ya kupanga vipaumbele pamoja na kuwa Wabunge wanaishi vijijini, wanakaa karibu kabisa na wananchi, na ndiyo wenye kujua vipaumbele katika maeneo yao. Wananchi nao wamewachagua kuwa Wabunge ili wawe sauti yao. Mfumo wa bajeti wenyewe hauko wazi, hivyo kuwanyima Wabunge na hata maafisa wahasibu kujua kwa uwazi mafungu ya matumizi na uingizwaji wa fedha za matumizi. Aidha utaratibu wa Cash Budget nao hausaidii tena, kwani sasa Serikali inajua kiwango cha mapato ya uhakika kwa mwezi, hivyo kambi ya upinzani inashauri yafuatayo yafanyike:-
- Kuwe na Kikao Cha Mipango, katika ngazi ya Wilaya, Mkoa kila Mwezi wa Novemba ili kuweka vipaumbele vya kiwiliya na Mikoa na hatimaye kufuatiwa na kikao cha wadau mwanzoni mwa mwezi wa January, kabla ya Kamati ya Mipango ya Bunge Mwezi wa January/Februari;
- Kupunguza, idadi ya Wizara zinazohudumia jambo moja, hasa kwa fedha zinazokwenda kwenye Halmashauri, kwa kukusanya fedha yote inayokwenda kwenye mradi au matumizi kwenye Wizara husika tu.(k.m.fedha za elimu-zinazotoka TAMISEMI, Maendeleo ya Jamii nk. zote ziingie TAMISEMI ziende Halamshauri). Wizara ya Elimu ibakie kusimamia Taaluma na kuwaandaa Waalimu tu.
- Kuachana na utaratibu wa Cash Budget na kurudisha utaratibu wa ‘Warant of Funds’. Utaratibu huu utawezesha Wizara/Halmashauri kutumia katika viwango vya bajeti bila ya kungoja fedha. (Afisa Muhasibu atakae tumia zaidi ya kiwango alichoidhinishiwa, adhabu yake ni kufukuzwa kazi bila ya onyo).
- Kupunguza gharama za uendeshaji kwa kupunguza ukubwa wa Serikali, kuratibu vyema safari za viongozi na watumishi, kupunguza magari ya anasa, na kwa kuzitumia zaidi ofisi zetu za kibalozi badala ya safari za viongozi na ofisi hizo kuangliwa upya mfumo wa matumizi yao ili yalingane na shughuli zilizoko katika ubalozi husika;
- Kuongeza Mabalozi wa Heshima katika nchi au miji ambayo nchi yetu inaweza ikaimarisha bishara hasa utalii na mauzo ya nje;
- Kupunguza idadi ya makampuni yaliyoko bandarini kwa kuipa jukumu TRA na kuiongezea uwezo wa kuitendaji na vifaa vya kisasa, aidha TRA kuingia ubia na makampuni yenye utaalamu maalum kwa njia ya “Puplic- Private Partnership” ili kukusanya kwa uhakika kodi katika maeneo ya Maliasili, Madini, Utalii,na kadhalika;
- Kuandaa operesheni maalum kwa ajili ya kupambana na wahalifu wanaotorosha raslimali zetu, kwa kushurikiana na nchi marafiki,kama vile China ambayo inanunua magogo na mbao nyingi kuliko zilizoko katika takwimu zetu;
- Kuongeza wigo wa kodi baada ya kuondoa kundi la wafanyakazi wanaosamehewa kodi. Kima cha chini kipande hadi kufikia Tsh215,000/ na kuongeza viwango vingine kwa asilimia inayolingana na mapato ya Serikali;
- Kupitia upya Mikataba yote ya ajira katika Sekta Binafsi ili kulinda maslahi ya wafanyikazi;
- Kuwawezesha Watanzania wajasiriamali ambao wako tayari kuwekeza kwenye viwanda vya vito ili kudhibiti usafirishaji wa mali ghafi ya vito;
- Kutathmini upya utekelezaji wa Sera ya Serikali kuhamia Makao Makuu Dodoma.
- Kuongeza bajeti ya maendeleo kwa kiwango kisichopungua asilimia 45 badala ya 36 ya Serikali mkazo vipaumbele vikiwa Elimu, Afya, Kilimo, Miundombinu na Utawala Bora.
- Kugawa mapato ya Muungano kwa kutumia asilima 15 ya mapato itakayoenda Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar badala ya 4.5 inayotokana na Misaada;
- Kuanzisha Bandari Huru yaani ‘Free Port’ Zanzibar kama njia ya Tanzania kuwa na ‘Dubai yake’, ili kupanua biashara ya kupitia nchini kwetu (transit trade).
- Kuondoa mara mmoja utaratibu wa Pre-Shipment Inspection unaofanywa na Makampuni ya nje na kazi hiyo kuwa chini ya TBS yenyewe na hivyo kuwaongezea mapato, kuwaondolea
usumbufu waagizaji, kuwapunguzia gharama waagizaji na kuongeza ajira.
- Kuwarahisishia Watanzania kwa kuifanya mamlaka ya manunuzi nchini ijitegemee kwa kutumia utaratibu wa manunuzi wa mtandao (e-Procurement) kwa ajili ya kusajili makampuni katika ngazi za wilaya, Mkoa hadi Taifa na nje zinazotoa huduma kwa Serikali. Kuiboresha mamlaka hii ili isaidie kupunguza rushwa katika manunuzi na kuipunguzia hasara Serikali ya wastani wa si chini ya 15% ya manunuzi yake yote.
IV. MAONI YA KAMBI YA UPINZANI JUU YA VIPAUMBELE VYA BAJETI
- Kupunguza Bajeti Tegemezi kutoka 42%-31.8%:
Mheshimiwa Spika, Katika mkutano uliopita wa Bajeti tulisema sana juu ya jambo hili la kutegemea wafadhili katika maendeleo yetu.Kambi ya Upinzani inaipongeza TRA kwa kukusanya mapato kwa kiwango marudufu kulingana na miaka iliopta.Lakini pia tulisema kuwa uwezo wa Serikali kukusanya mapato ni mkubwa zaidi, ila kuna uzembe mkubwa na kutojali (laxity), ubadhirifu, na ufisadi kama inavyodhihirishwa na Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali mwaka hadi mwaka. Madhara ya Bajeti ya namna hii ni kwamba tunapopata matatizo inabidi kupita pita (reallocation) na kupunguza matumizi kadhaa ili tu kuweka hali sawa ya madhara yaliotokea. Hii ni hatari kwa Maendeleo kwa Watanzania kwa kiasi kikubwa kwani hata bajeti ya mwaka huu baadhi ya Wizara zilipunguziwa fedha bila mpangilio. Mathalan, Mwaka wa fedha umepita hakuna hata barabara moja mpya iliyofunguliwa.
Kambi ya Upinzani, inaomba kupendekeza njia ambazo itapunguza utegemezi kutoka asilimia 42% ya sasa hadi asilimia 31% kutokana na njia za mapato kama inavyoelezwa hapa chini.
- Kuongeza Mapato yanayotokana na Mali Asili:
- Mapato yatokanao na raslimali za Baharini na kwenye Maziwa;
Uvuvi katika bahari kuu
Mheshimiwa Spika, Uvuvi katika Bahari Kuu ni moja ya maeneo ambayo kama Serikali ingelikuwa makini na kuchukua maamuzi tunayopendekeza,mapato ya Serikali yangaliongezeka marudufu bila kugusa mafuta. Meneo yenyewe ni kama yafuatayo:-
-
Kuongeza ada ya leseni kwa meli za nje zinazovua katika bahari kuu hadi kufikia USD100, 000 kutoka, inayotozwa sasa ambayo ni USD18, 000 kwa mwaka. Somalia ambako kwa muda mrefu hakukuwa na Serikali wanatoza USD100, 000 kwa leseni. Kulingana na takwimu zilizopo ni kuwa kuna meli 140 (japo Kumbukumbu za Bunge-Kikao Cha tatu 5th.Feb.2004 Serikali ilisema kuwa imetoa leseni 193 za Meli za Uvuvi) za nje zilizopatiwa leseni za uvuvi katika bahari kuu ya Tanzania. Kwa maoni haya mapato ya yatakuwa Tshs 19bn. Ambayo sasa hayakusanywi.
- Kuongeza tozo la mrahaba wa mauzo la asilimia 10%.katika bidhaa za Samaki zinazovuliwa katika Bahari Kuu. Kila meli kwa mwezi inavua wastani wa tani 2000 za samaki, kwa makisio ya chini sana, japo kwa kawaida wanavua Tani 1,500 kwa siku.Bei ya soko kwa kilo ya samaki ni USD2.5 . Kwa wanaojua biashara ya sekta hii, kiwango cha uvuvi ni kikubwa zaidi. Kwa maoni haya Mapato yatakuwa shs. 740 bn. ambayo sasa hayakusanywi na Serikali.
- Katika kuhakikisha kuwa sekta hii ya uvuvi inaleta mabadiliko ya kiuchumi kwa nchi na wananchi kwa ujumla Bandari ya Mtwara,Dar es Salaam na Zanzibar inashauriwa zitenge maeneo ya bandari za samaki (Fish Ports and Fish Processing plants) ili meli zote za uvuvi wa bahari kuu zilazimike kununua mahitaji yao yote ya mafuta ,maji,chumvi na vyakula wanapo kuja kukaguliwa kwa ajili ya kukusanya mapato. (Vyombo vyetu vya ulinzi,vikishirikiana na TRA na Mamlaka ya Uvuvi kudhibiti mapato haya) Kwa uamuzi huu mapato yatakuwa Tshs.3bn. ambayo nayo sasa hayakusanywi na Serikali;
- Uvuvi katika maziwa ya Lake Victoria na Tanganyika, haujadhibitiwa vizuri.Hivi sasa kuna uvunaji haramu wa wastani wa Tani 36,000 kwa mwaka katika maziwa hayo matokeo yake viwanda vyetu vinakosa mali ghafi.Tunashauri hatua ya dharura kuikabili hali hii kwa kutumia vyombo vya ulinzi na TRA ili kuongeza mapato na ajira. Zoezi hili litaongeza wingi wa samaki hivyo viwanda vya samaki vitaongeza uzalishaji na kodi itaongezeka. Hatua hii ni ya kuongeza uwezo haitegemewi kwa kuingiza mapato. Serikali imeshindwa kushughulikia jambo hadi leo.
Mhe. Spika, Maoni haya Kambi ya Upinzani sio tu yamepanua wigo wa kodi, lakini pia kwa hatua hizo tutakuwa tumedhibiti uvunaji wa raslimali zetu ambapo sasa hazivunwi kikamilifu.
- Mapato yanayotokana na Misitu
Mheshimiwa Spika, Chanzo kingine kikubwa ambacho vile vile mapato yake hayakusanywi sasa na Serikali katika sekta ya maliasili na hasa bidhaa za magogo na mbao.
Kutokana na ripoti za kiutafiti kutoka kwa kundi la wahisani na pia Asasi kadhaa zisizo za kiserikali, (Kama TRAFFIC) (2005/2006) Serikali ilikusanya asilimia 4 tu ya mapato kwa mwaka 2004 yaliyopaswa kukusanywa kutoka katika bidhaa za magogo na mbao. Wanunuzi wakubwa ni China, India na Japan. Katika utafiti huo, katika kipindi cha 2001/2005 China peke yake ilinunua Cu.mita 18,316 x $150 kwa rekodi za Maliasili Tanzania kwa bei ya wastani wa USD2.7m. sawa na Tshs. 3.5bl. na CU.mita 108,605 kwa rekodi za Forodha za China, kwa maana hiyo ama kwa ufisadi au vyenginevyo Serikali imekosa mapato ya Cu.mita 90,289 x $450 = $40.6m. sawa na Tshs.52.8bn. utafiti huu ulihusu Magogo na mbao zinazotoka Mikoa ya Kusini tu. Taarifa hii inathibitisha Taifa lilikoseshwa fedha kwa kuuza kwa Dola 150 tu wakati bei halisi China ilikuwa Dola 450. Pia kiwango kilichouzwa kimefichwa. Huu ni Ufisadi.
Mheshimiwa Spika,Kambi ya Upinzani inashauri hatua zifuatazo zichukuliwe:-
-
Halmashauri za Wilaya zilizo katika maeneo ambayo bidhaa hizi zinap matikana ziwe mawakala wa kukusanya mapato kutokana na bidhaa za maliasili. Uamuzi huu utapunguza kwa kiasi kikubwa ufisadi uliopo sasa katika Wizara ya Maliasili. Kila Halmashauri inayokusanya kodi ipatiwe gawio kutoka sehemu ya makusanyo;
- Mapato yote yakusanywe na TRA kwa kutumia stakabadhi za TRA kupitia Halmashauri za Wilaya kama ilivyo elezwa hapo ju;
- Mtu yeyote atakayekamatwa kwa kutorosha maliasili afilisiwa kwa mujibu wa sheria kama haipo itungwe;
- TRA mbali na kukusanya mapato ishirikiane na Bodi ya Mauzo ya Nje kuhakiki bei za Bidhaa zetu zinazouzwa nje ili kupata mapato halali ya Rasilimali zetu.
Mhe. Spika, Kwa hatua hizi mapato ya maliasili misitu yataongezeka kwa asilimia 90 ya mapato ya sasa, makusanyo halisi yatakuwa Tshs 100bn ambazo hazikusanywi sasa.
- Mapato yatokanayo na Utalii:
Mhe. Spika, Serikali inaona kuwa inakusanya mapato kwa wingi hadi kufikia asilimia 16.8% ya pato la Taifa katika Sekta hii. Hata hivyo, Serikali imeshindwa kufikia malengo ya watalii milioni moja kwa mwaka kama ilivyokuwa imepanga.Idadi ya watalii wanaokuja nchini ni wastani wa laki sita (644,124). Isitoshe, Serikali imekuwa ikipoteza mapato kutokana na watalii kulipia gharama za safari zao na baadhi ya huduma kwa Tour Operater huko huko kwao kwa wastani wa USD200-300 kwa mtu mmoja kwa siku. Mtalii anapo fika Tanzania ,huwa analipa wastani wa USD80-150 tu. Hivyo kuzipunguzia mapato hoteli zetu na kwa maana hiyo na Serikali.Kama nusu ya watalii hawa(322,062) kuwa wanakuja katika “Packege Tour” na kuwa tunakusanya wastani wa USD100 kwa siku kwa kila mmoja kwa muda wa siku 7., ukiacha mapato yasio ya moja kwa moja,katika eneo hili Serikali inglikusanya kama kodi ya mapato 30% sawa ma Tshs.67.5bn ambazo hazikusanywi hivi sasa.
- Mapato yatonayo na Uwindaji:
Mhe.Spika, Kwa mujibu wa takwimu za Maliasili, kuna vitalu 152. Kwa wakati huu Serikali inakodisha kwa wastani wa USD7500=kwa mwaka (mara nyingi wamiliki nao hukodisha kwa wenye fedha kwa wastani wa USD100,000.kwa mwaka) Ili kuongeza mapato ya Serikali, Kambi ya Upinzani inashauri hatua zifuatazo zichukuliwe ili kuongeza mapato kama ifuatavyo :-
- Kuwajasirimisha Watanzania vitalu vyote vya uwindaji;
- Ili kupata thamani halisi washauriwe kuingiza Vitalu hivyo katika soko la mitaji kwa kutumia”eletronic commerce.”;
- Kupandisha viwango vya kodi ya Uwindaji;
- Kutoza asilimia 30% ya mapato yatokanayo na Mtanzania atakayekodisha kwa mtu mwingine.
Kwa hatua hii Watanzania watakuwa wamewezeshwa kumiliki rasilimali zao wenyewe na pia kwa kuongeza viwango vya kodi ya uwindaji makusanyo yanakisiwa kuwa Tshs. 85bn ambayo hayakusanywi hivi sasa.
- Mapato katika Sekta ya Madini
Mheshimiwa Spika, Katika sekta ya madini, kwa kulingana na ukaguzi uliofanywa na Kampuni ya Alex Stuart, kwa kipindi cha miaka mitatu Serikali imepoteza shillingi 1.3 trillion. Na hii imetokana na Serikali kutokuwa makini katika kufuatilia nyaraka halali zinazotumiwa na makampuni ya kuchimba madini.
Ili kuifanya sekta hii ya madini kuwa na manufaa kwa Taifa na Watanzania wote hatua zifuatazo zikichukuliwa sekta hii itachangia zaidi:-
-
Kufanya mapitio ya sheria ya madini na kupandisha asilimia ya mrahaba toka 3% hadi 5% kwa kuanzia;.
- TRA kuimarishwa kiutendaji na kukusanya kodi zote katika sekta ya madini;
- Katika mpango wa maendeleo wa kampuni husika, maendeleo ya jamii zinazozunguka migodi yaonekane wazi wazi na kuingizwa katika mpango wa mwekezaji;.
- Kati ya asilimia 5% za mrahaba utakaotozwa asilimia 2% iabaki katika Halmashauri ya Wilaya/Mji ambamo mgodi upo.
- Katika masharti ya kuwekeza kwa wageni,ni lazima waingie ubia na Mtanzania au Halmshauri angalau kwa asilimia 10% ikiwa ni pamoja na thamani ya ardhi.
- Kuweka sharti ndani ya Mikataba na kubadilisha sheria kwamba atake kiuka mkataba au kusafirisha mali itokanayo na raslimali za nchi kampuni husika itafilisiwa;
- Kuhakiki madeni waliyokopa wawekezaji ili kupata kiasi halisi walichokopa, ikiwa ni pamoja na Tax Holiday kwa lengo la kufuatilia muda wa Kusamehewa Kodi.
Mheshimiwa Spika, kwa kutumia taarifa ya kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, na tukichukua wastani wa mapato tunayopoteza kwa mwaka Katika sekta hii,Serikali ingelikusanya jumla ya shillingi 433bn kwa kuziba tu mianya ya kukwepa kodi. Vile vile kutokana na uamuzi wa kupandisha mrahaba Serikali ingekusanya jumla ya shilingi 41.8billion kutokana na mauzo ya madini, hasa dhahabu.
Mapato kutoka madini ya Vito
Mheshimiwa Spika, Taarifa mbalimbali za kitafiti zinaonesha kuwa Tanzania inapoteza mapato mengi sana katika madini ya vito kwa sababu ya uzembe na ufisadi. Kwa mfano, Katika soko la dunia mauzo ya Tanzanite mwaka 2005 yalikuwa na thamani ya Dola za kimarekani 400m. Hata hivyo rekodi ya Tanzania ni Dola 16m tu.Tuna taarifa kuwa Kenya ilipata tuzo kwa kusafirisha Tanzanite nyingi duniani wakati hawana Tanzanite.
Mheshimiwa Spika, kama Serikali ingekubaliana na ushari wa Kambi ya Upinzani, Serikali ingepitia upya kabisa mwenendo mzima wa biashara ya madini haya ili kuwa na chanzo kimoja tu cha mauzo. Udhibiti huu ungipatia Serikali mapato ya jumla ya Tshs. 100bn. ambayo haikusanywi hivi sasa.
- Mapato katika Kodi Nyinginezo
- Misamaha ya Kodi
Mheshimiwa Spika, eneo lingine ambalo tumekuwa tukipoteza fedha nyingi sana ni eneo la misamaha ya kodi. Kama ilivyo katika taarifa ya kamati ya fedha na uchumi ya Bunge, inakadiriwa kuwa takribani shilingi 673billion zilitolewa kama misamaha ya kodi katika mwaka wa fedha unaomalizika. Ili kuongeza mapato yetu ya ndani Kambi ya Upinzani inashauri Serikali ipunguze misamaha ya kodi kwa asilimia 50%. Uamuzi huu mapato yatakuwaTsh 336.5bn ambazo hazikusanywi hivi sasa.
- Kodi katika Posho ‘ALLOWANCES’
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa sheria ya kodi ya mapato, sheria na.11 ya mwaka 2004 kifungu cha 7(1) na (2) , kila atakachokitoa mwajiri itabidi kikatwe kodi isipokuwa kama mfanyakazi atatumia fedha zake na mwajiri akamrudishia. Kwa mujibu wa sheria hii posho zote za warsha, semina, makongamano, mikutano na vikao zinapaswa kukatwa kodi ya mapato. Hii pia inajumuisha posho wanazopata Waheshimiwa Wabunge kutokana na vikao hapa Dodoma na Dar es Salaam.Ikirekebishwa sheria ya kodi ili kutoza kodi mapato haya kwa kiwango cha VAT yaani 20%. Hatua hizi pia ingelenga kupata manufaa yafuatayo:-
- Mifuko ya Pensheni itapata wanachama zaidi.
- Kodi ya Serikali ambayo ni ya uhakika (P.A.Y.E. itapanda maradufu kwani employment allowance haitozwi).
- Wafanyakazi watakuwa na kipato kitakachowapa moyo wa kufanya kazi hivyo kuongeza ufanisi kazini.
Mhe. Spika, uamuzi huu Serikali ingepata mapato ya Tshs.8bn ambazo hazikusanywi hivi sasa.
- Mauzo ya hisa za NMB
Mheshimiwa Spika, eneo lingine linaloinyima Serikali mapato yake ni uuzwaji wa hisa zake kwa bei isiyokuwa ya soko.Kwa mfano hisa 25% za Serikali za Wiilliamson Daimond ziliuzwa kwa USD 183,000 tu. NIC,ilitaka kubinafsishwa kwa thamani ya Ths3bn tu,hadi Kamati ya Fedha na Uchumi ilipodai tathmini mpya, kulingana na tathmini mpya iliyofanywa na Chuo Kikuu kishiriki cha Ardhi. thamani imepanda hadi Tshs.6bn.Hisa za NMB zinatarajiwa kuuzwa kwa Tshs. 15bn. Kiwango hiki ni cha chini kulingana na. NMB ni benki inayopata faida sana na imeweza kutoa gawio kwa wanahisa.Kambi ya Upinzani inashauri Serikali kuuza hisa za NMB kwa bei ya soko.Kwa ushauri huu Mapato yatakuwa Tshs 45 billioni badala ya 15 Billioni ongezeko la Billioni 30.
- Mapato kutokana na Bandari ya Mtwara
Mheshimiwa Spika, Eneo lingine ambalo bado halijatumiwa vizuri na la kuuza mauzo nje ya nchi na hasa nchi jirani(Bonded Goods).Kama bandari ya Mtwara ingejengewa maghala ya kuhifadhia mazo na bidhaa kwa kufanya mauzo ya bidhaa zetu za viwandani kama vile cement na mifugo,mchele na bidhaa nyengine katika nchi ya Comoro, ambayo matumizi yao kwa mwaka, cement kwa mwaka Mt70,000,Mchele 40,000,ngombe ni 4000 kwa wiki, ambayo inaitegemea sana Tanzania katika vyakula na vifaa vya ujenzi. Aidha tutasukuma uuzaji wa bidhaa zetu nje kama Muhogo,korosho,ufuta na samaki. Uimarishaji huu utaweza kutuingizia kiasi cha shilingi 2billioni kutokana na kodi peke yake ambayo sasa haikusanywi.
- Kodi ya ongezeko la thamani
Mheshimiwa Spika, mwaka jana Serikali ilifuta kodi ya VAT katika mafuta ya petrol. Uamuzi huu haukuleta matarajio ya unafuu kwa mwananchi wa kawaida.Kambi ya upinzani inashauri kuwa irudishwe VAT katika eneo hili na hivyo kupata mapato ya Tshs. 153billion bila athari kwa mwananchi wa kawaida.
- Kodi itakayo tokana na Leseni za Madereva
Mheshimiwa Spika,Kambi ya Upinzani inashauri kuwa mfumo wa leseni za madereva uboreshwe kwa kutoa leseni mpya kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya komputa. Leseni hizi zitakuwa na uwezo wa kuhifadhi taarifa zote muhimu za madereva. Hii itasaidia kupunguza uhalifu na hasa ajali za barabarani na pia itakuwa ni sehemu ya kitambulisho. Mradi huu uendeshwe kwa utaratibu wa PPP.Kwa makisio ya chini, madereva laki mbili na nusu mwaka huu wa fedha na ada ya leseni kuwa shs. 50,000, tutakusanya jumla ya shilingi 12.5bn ambazo sasa hazikusanywi.
- Mapato kutokana na kuuza ndege ya Rais
Mheshimiwa Spika, kutokana na dhamira yetu toka mwaka 2003 kwamba ununuzi wa ndege ya Rais ni anasa na gharama zisizo na msingi kwa sasa Serikali inatumia Shs 6 Millioni kwa saa ya kuruka ndegehii.Kambi ya Upinzani bado inaendelea na ushauri wake kwamba ndege hii kama alivyofanya Rais wa Ghana Bw. John Kufouri iuzwe kwa mnada. Kwa uamuzi huu Serikali itapata mapato Tshs 35billion.
Mheshimiwa Spika,ushari huu uliotolewa na Kambi ya Upinzani,kama Serikali ingekubali kuufanyia kazi kuhusu sera ya mapato, yangeipatia Serikali jumla ya mapato ya ziada ya Tsh. 2,181.3 bn.Ushauri wa Mapato haya yote ni kutokana na kuboresha Vianzio vilivyopo na Kubuni vipya ambayo Serikali haikuviona.
Mhe.Spika,muhtasari, wa ushari wetu juu ya MAPATO ya Serikali ni kama ifuatavyo:-
| Na. |
Mapato |
Kiasi (TShs) Bilioni |
1 |
Ada za leseni za meli zinazovua bahari kuu |
19 |
2 |
Mrahaba kutokana na Uvuvi katika bahari kuu |
740 |
3 |
Mapatao kutokana na mafuta kwa meli za uvuvi |
3 |
4 |
Mapato kutokana na bidhaa za misitu |
100 |
5 |
Mapato kutokana na biashara na Comoro kupitia bandari ya Mtwara |
2 |
6 |
Mapato kutokana na punguzo la 50% ya Misamaha ya kodi |
336.5 |
7 |
Kodi ya 20% kutokana na posho za semina nk. |
8 |
8 |
Mauzo ya hisa za Serikali i.e. NMB |
45 |
9 |
Ukusanyaji wa kodi isiyokusanywa kwenye madini |
433 |
10 |
Ushuru wa mauzo kutokana na madini ya Vito i.e. Tanzanite |
100 |
11 |
Mapato kutokana na Vitalu vya Uwindaji wa Kitalii |
85 |
12 |
Mrahaba wa asilimia 5 katika madini |
41.8 |
13 |
VAT katika mafuta ya petroli na dizeli |
153 |
14 |
Mauzo ya Ndege ya Rais |
35 |
15 |
Mapato kutokana na leseni za madreva |
12.5 |
16 |
Mapato kutokana na utalii |
67.5 |
|
Jumla |
2,181.3 |
Mheshimiwa Spika, Katika bajeti iliyosomwa na Mheshimiwa Zakia Meghji mnamo tarehe 14 Juni 2007, Serikali inapendekeza kurekebisha baadhi ya viwango vya kodi na tozo nyingine za kodi chini ya sheria mbali mbali ambazo zingeiingizia jumla ya shilingi billioni 239.161 . Kutokana na ushauri wetu, tunapendekeza kodi na ushuru uliotumika mwaka 2006/07 usibadilike isipokuwa kodi ya ongezeko la thamani katika bidhaa za mafuta ya Petroli.
Mheshimiwa Spika, Kwa ushauri wetu wa mapendekezo yetu ya mapato tungeweza kukusanya jumla ya shs. 5.3tr kama mapato ya ndani. Makusanyo haya yangekuwa ni ziada ya makusanyo ambayo Serikali imepanga kuyakusanya kwa kiasi cha shs. 1.8tr. Tofauti ya zaidi ya Trillion 5 na bila kumuumiza mwananchi wa kawaida.
Mheshimiwa Spika, Tukizingatia kuwa nchi yetu itapata misaada na mikopo kutoka nje kama jinsi ambavyo imeainishwa katika Makadirio ya Bajeti ya Serikali ya mwaka 2007/2008, Makadirio ya Mapato ya Bajeti hii yangefikia jumla ya Tshs. 7.99Trilion.
V. MAONI YA KAMBI YA UPINZANI KATIKA MATUMIZI
Mheshimiwa Spika, Katika kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata matunda ya kile kinachokusanywa,Serikali ingeweka mkazo katika maeneo yafuatayo:-
- Mishahara kwa watumishi wa Serikali
Mheshimiwa Spika, Kutokana na kuongezeka kwa mapato ya ndani,Kambi ya Upinzani inashauri kiwango cha chini cha Mshahara Wa wafanyikazi wa Umma kiwe Tshs 215,000/ kwa mwezi, kwa ngazi nyingine mshahara ungepanda kwa asilimia ambayo italeta uiwiano baina ya kipato cha chini na cha juu. Ufafanuzi wa kina wa utatolewa na Waziri Kivuli wa Utumishi wa Umma.
- Elimu
Mheshimiwa Spika, Elimu ni kipaumbele chetu kikuu katika matumizi ya Serikali. Hata hivyo sekta ya elimu inapaswa kutengewa fedha zaidi ili kuboresha elimu.Kwa maoni ya Kambi ya Upinzani nikuwa Serikali imejikita zaidi katika hatua ya awali kuwa na shule nyingi,idadi kubwa ya wanafunzi,jambo ambalo limefanikiwa vizuri sana.Hongereni.Kutokana na kazi kubwa iliofanywa na Kambi ya Upinzani ya kutafuta mapato zaidi,muono wetu ni kuimarisha hatua iliofikiwa kwa kuelekeza matumizi yetu katika kuboresha viwango vya elimu ili kuwa na ELIMU BORA Hivyo, tunashauri,kuwa tuhakikishe mkazo mkubwa unawekwa katika kuwaelimisha walimu,katika ule mtindo wa zamani.Kwa kuwa hivi sasa tuna upungufu mkubwa wa Walimu kufuatia ujenzi wa Shule za Sekondari za Kata, Serikali yetu ingeajiri walimu kwa muda kutoka nchi jirani za Kenya, Uganda, Malawi, Zimbabwe Zambia na India. Utaratibu huu ungedumu kwa miaka miwili ambapo tutakuwa tayari tumehitimisha walimu wapya,tumetafuta vifaa vya kufundishia pamoja na vitabu na nyumba za walimu kuwa katika hadhi inayokubalika ili kurejesha heshima ya mwalimu katika jamii.
-
Tusingejali chochote katika kuhakikisha watoto wetu wanapata elimu bora. Uamuzi huu usingekuwa na tatizo lolote kwani Watanzania wengi sana walienda kufundisha katika shule za nchi hizi wakati wao wakiwa na shida. Mfano, kumbukumbu zinaonesha kuwa, Mheshimiwa Bujiku Sakila alikuwa mwalimu huko Msumbiji baada ya uhuru wa nchi hiyo mwaka 1975.
- Mhehismiwa Spika, Kambi ya Upinzani inaona kuwa, mtazamo wetu ungekuwa katika kuweka shule kuwa rafiki wa mwanafunzi kwa kuboresha majengo. Katika ujenzi wa nyumba za walimu tungetumia teknolojia wa “Pre-fabricated houses” ambayo ni rahisi na haraka. Katika kuendeleza Teknolojia hii na pia ujenzi huu wa nyumba za Walimu, viwanja vya michezo, mabweni na maabara Majeshi yetu ya Magereza na JKT kupitia mashirika yao ya ujenzi,yaingie ubia na makampuni ya nje kwa utaratibu wa PPP ikiwa pia ni hatua ya kupata utaalamu ambao utapunguza kwa kiwango kikubwa ujenzi wa nyumba zao pia.
- Mheshimiwa Spika, kwa maoni ya Kambi ya Upinzani Serikali ingetenga asilimia 20 ya bajeti yote katika Elimu kama ilivyo katika bajeti hii ingeweza kwa kiwango kikubwa kuwa na Elimu Bora. Maelezo zaidi katika matumizi yetu katika Elimu ya Msingi na Sekondari yatafafanuliwa na Waziri Kivuli wa Elimu.
- Elimu ya Juu
Mheshimiwa Spika, Katika kuhakikisha kuwa wanafunzi wetu wanapata elimu ya juu na ilio BORA,Kambi ya Upinzani inashauri kuwa, wale wote watakaopata udahili katika vyuo vyetu vya elimu ya juu wapate mkopo kwa asilimia mia moja (100%). Katika kuhakikisha kuwa mikopo itakayotolewa inakuwa ni kwa Watanzania tu, vyombo vya fedha ndivyo vihusike na utoaji wa mikopo na bodi ibaki na kazi ya kutoa miongozo na taratibu tu. Wanafunzi wote watakiwe kufungua Bank Account na TIN kwa udhibiti na uhakika wa marejesho pia kuongeza wigo wa walipa kodi.
Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani,inashauri kuwa ili kuongeza ushindani wa kupata ubora wa wahitimu, uewekwe utaratibu ambao ungegeuza sehemu ya mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu kuwa misaada i.e grants kulingana na viwango vya kufaulu katika mitihani ya mwisho wa mwaka.
Mheshimiwa Spika,Ushauri juu ya utaratibu gani utatumika katika kuteua asasi za kifedha zitakazotumika kutoa mikopo na vile vile jinsi ya kugeuza mkopo kuwa grant utatolewa na Waziri Kivuli wa Elimu ya Juu.
- Kilimo
Mheshimiwa Spika,Ushauri wetu katika Kilimo, inalenga kuboresha Kilimo na hivyo kuhakikisha kinakua kwa asilimia 8 kwa mwaka. Tunashauri yafuatayo:-.
- Tuhakikishe kuwa wakulima wetu wanalima kwa ajili ya soko, hivyo ubora na wingi wa bidhaa iwe ni agenda muhimu kwa upande wetu. Ili kupata bei nzuri katika soko tuweke mazingira bora kuhakikisha mazao yataongezwa thamani kabla ya kuuzwa (add value through processing;
- Pamoja na mazao mengine tujitahidi kuhimiza kilimo cha mazao ambayo yatatupatia nishati mbadala kwa lengo la matumizi ya nishati hiyo katika kukifanya kilimo kuwa cha kisasa kwa gharama nafuu;
- Tuimarishe “rural infrastructure” ambayo itasimamiwa na “rural road agency” na barabara hizi ziwe zinapitika mwaka mzima;
- Vyuo vyote vilivyokuwa vinatoa mafunzo na elimu ya kilimo kuanzia ngazi ya chini vitafufuliwa. Jambo hili litaongeza wataalam wengi wa Ugani ambao watakuwa na taaluma kulingana na zao husika na eneo husika;
- Kutafuta tekinologia( Hygrex) inayoweza kukausha na kuhifadhi mazao hasa matunda kwa ajili ya soko la nje hasa Marekani ya Kaskazini na Arabuni;
- Kuainisha na kuwanisha(integrate) viwanda vinavyo tumia malighafi za kilimo ili kuongeza thamani ya mazao yetu nje na kuongeza bei kwa mkulima;
- Kuhakikisha kuwa wakulima na wafanyi biashara wanapata taarifa sahihi za bei za Bidhaa katika masoko ya ndani na ya nje ya nchi kwa kutumia vyombo vyote vya habari nchini kwa muda maalum;
Mheshimiwa Spika, bajeti hii imepanga asilimia 12 % ya Bajeti yote kwa ajili ya kilimo badala ya asilimia 6.2 % iliyotengwa na serikali katika Kilimo. Maelezo juu ya ushauri wa matumizi wa miradi ya maendeleo atayatoa Waziri kivuli wa Kilimo.
- Afya
Mheshimiwa Spika,Kutokana na vyanzo vipya vya mapato vilivyobuniwa na Kambi ya Upinzani, ili kuhakikisha kuwa tunajenga jamii yenye afya, itakuwa ni jukumu la Serikali kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wa elimu ya msingi na Sekondari wanapimwa afya zao bure (preventive health care) , jambo ambalo litasababisha kuwapa hamasa wazazi wao ili na wao kuwa na utaratibu wa kupima afya zao.Serikali ihakikishe madawa yakutosha yana kuwepo kuanzia katika ngazi ya Zahanati mpaka kwenye Hospitali.Kwa kutumia utaratibu ule ule wa kutumia Pre-fabricated tekinologi, zahanati zitajenwa sambamba na matayarisho ya wataalam , ili kuepuka raia kupoteza maisha kwa ukosefu wa mtaalamu.( Ukikosa mwalimu mtoto atajua kucheza na wenzake,ukikosa mtaalamu wa utibabu utapoteza maisha). Utaratibu huu unalenga uwiano mzuri wa huduma, mipango sahihi na siyo maamuzi ya kisasa ambayo siyo endelevu.
Mheshimiwa Spika, tumetenga asilimia 9% ya bajeti hii kwa ajili ya sekta ya afya. Maelezo zaidi juu ya matumizi ya kiasi hiki kilichotengwa atayatoa waziri kivuli anayehusika na sekta hiyo.
- Miundombinu
Mhe.Spika,Kambi ya Upinzani,baada ya mchakato wa kupata njia za kupata mapato mapya ya ndani, inashauri kuwa asilimia 21 ya mapato ipewe sekta hii na lengo kuu liwe ni kutengeneza barabara kuu za kuifungua Tanzania kiuchumi.,aidha tunashauri kuwa katika utaratibu wetu wa ujenzi umuhimu uwekwe katika ujenzi wa barabara kwanza na sio kwa madaraja kama inavyofanyika sasa, barabara za kipaumbele ziwe kama zifuatazo:-
- Masasi-Tunduru-Songea,
- Tunduma-Sumbawanga-Mpanda-Kigoma
- Manyoni – Itigi – Tabora – Kigoma
- Iringa – Dodoma – Babati
- Mbeya – Sikonge –Tabora- Nzega
- Babati –Singida
- Oldeani-Matala- Lalago
Mhe. Spika, Kwa kutengeneza barabara hizi tutakuwa tumeifungua milango ya biashara kwa Tanzania nzima, hivyo basi bandari za Mtwara na Kigoma zitakuwa ndio injini za mapato kwa nchi hii kutokana na uzalishaji kwa mikoa inayozunguka mikoa hiyo ya Mtwara na Kigoma.Ili kuhakikisha kuwa miradi ya miundombinu haikwami,na kama kweli Serikali inataka mbadiliko ya haraka ibainishe miradi inayotaka kuendeshwa kwa BOT na PPP ili kurahisisha uwekezaji katika eneo hili Mhe.Spika, wawekezaji wengi wamekuja kwa njia ya BOT na PPP lakini hadi leo hakuna maamuzi.
- Nishati
Mhe. Spika, Katika Sekta hii tumetenga asilimia 8% ya bajeti yetu kivuli. Tunaishauri serikali ihakikishe kuwa uzalishaji wa umeme wa maji toka Stigglers Gorge unazalishwa ili kuondokana na kutegemea umeme wa bwawa la Mtera ambalo uwezo wake unapungua kutokana na sehemu kubwa ya bwawa kujaa tope.
Mhe. Spika, Kambi ya Upinzani inalenga kushauri kupata nishati mbadala inayotokana na uzalishaji wa kilimo (Bio-energy). Katika mchakato huo wa uzalishaji nishati bidhaa kadhaa zitapatikana bila kusahau mbolea (organic fertilizers). Jambo litakalo inua kilimo hai kwa Watanzania.Ina shauriwa kila Mkoa uwe na mradi wake wa kuzalisha umeme wa kutumia Bio-energy na Tanesco iwe na jukumu la uratibu na usambazaji tu.ushauri huu utasaidia sana kupunguza gharama za uzalishaji na kuongeza idadi ya wananchi wanatumia umeme,ikiwa pia ni hatua ya kuhifadhi mazingira.
Mhe. Spika,Kambi ya Upinzani,inaona umuhimu wa kufufua utaratibu wa kusafisha mafuta (Refinery) ili kupata lami ambayo itatumika kujengea barabara na bidhaa zinazotokana na mafuta. Wapo wawekezaji wengi walikuja kuomba mradi huu lakini bado anatafutwa “stretegic invester”.
Mheshimiwa Spika, Kwa umuhimu wa pekee tunashari Serikali iifanye Mikoa yote ya Pwani bila ya kuisahau Mafia kuwa wazalishaji wakuu wa “Biofuel” kutokana na kuwa ni wazalishaji wakuu wa zao la nazi. Kwa umuhimu huo kunahaja ya kuhakikisha uchumi binafsi kwa wananchi wa Mikoa ya Pwani unakuwa kwa vile itakuwa ni sehemu nzuri kwa kilimo cha Mibono (Jatropha).ambacho soko lake liko juu sana .(Usd 350 kwa tani).
VI. USHAURI WA KAMBI YA UPINZANI JUU YA UTARATIBU WA MGAO WA KUTUMIA FEDHA
Mheshimiwa Spika, kama tulivyoshauri katika hatua mbali mbali za maoni yetu, katika kutekeleza mipango yake Serikali, na kuwafanya watekelezaji wa mipango hiyo waweze kutekeleza vyema,, utaratibu wa “cash budget” haufai. Utaratibu uliokuwa unatumika zamani wa ”Warrant system”urudiwe. Aidha Fedha badala ya kutolewa kwa mtindo wa kila mwezi, utaratibu wa kutoa fedha kwa kipindi cha miezi mine mine utumike.
Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa vipaumbele tulivyo shauri, tumegawa mapato kama ya bajeti hii kivuli kama ifuatavyo:-
| |
Sekta |
Asilimia |
Shilingi (Bilioni) |
| 1 |
MiundoMbinu |
21% |
1,678.734 |
| 2 |
Elimu |
20% |
1,598.794 |
| 3 |
Kilimo |
12% |
959.277 |
| 4 |
Afya |
9% |
719.457 |
| 5 |
Nishati |
8% |
639.518 |
| 6 |
Maji |
7% |
559.578 |
VII. USHAURI WA KAMBI YA UPINZANI JUU YA SURA YA BAJETI
| |
Mapato: |
|
A. |
Mapato ya Ndani |
5,399.722 |
B. |
Mikopo na Missada ya Nje ikijumuisha HIPC/MDRI |
2,549.249 |
C. |
Mauzo ya Hisa za Serikali |
45.000 |
|
|
7,993.971 |
|
Matumizi: |
|
D. |
Matumizi ya Kawaida |
3,940.213 |
|
1) |
Mfuko Mkuu / CFS |
615.039 |
|
|
2) |
Wizara |
2,410.751 |
|
|
3)
|
Mikoa |
86.704 |
|
|
4)
|
Halmashauri |
827.719 |
|
E. |
Matumizi ya Maendeleo |
4,053.758 |
|
(i) |
Fedha za Ndani |
2,591.866 |
|
|
(ii) |
Fedha za Nje |
1,461.892 |
|
|
Jumla ya Matumizi yote |
7,993.971 |
Mheshimiwa Spika, kutokana na mchanganuo huo, tofauti za kimsingi za hoja ya Waziri wa Fedha na Ushauri wa Kambi ya Upinzani ni kama ifuatavyo:-
-
Ushauri wa Kambi ya Upinzani kupitia bajeti hii kivuli utaiwezesha Serikali kutumia fedha za ndani asilimia 48% kwa ajili ya maendeleo, badala ya asilimia 21% tu iliyo wasilishwa na Serikali;
- Ushauri wa Kambi ya Upinzani kupitia bajeti hii kivuli utaiwezesha Serikali kutumia kiasi kisichopungua asilimia 45% ya bajeti yote kwa ajili ya maendeleo, badala ya asilimia 36% tu iliyo wasilishwa na Serikali.
- Ushauri wa Kambi ya Upinzani kupitia bajeti hii kivuli utaiwezesha serikali kupunguza Bajeti tegemezi. Mikopo na misaada toka kwa wahisani ni asilimia 31.8% ya bajeti nzima kivuli badala ya utegemezi wa asilimia 42% uliowasilishwa katika bajeti ya Serikali. Kwa ujumla bajeti yetu imepunguza utegemezi kwa kulinganisha na bajeti ya serikali kwa asilimia 10.2%.
VIII. MWISHO
Mheshimiwa Spika, Lengo kuu la Ushauri wa Kambi ya Upinzani kupitia bajeti hii kivuli niliyowasilisha ni kuchochea ukuaji wa uchumi, kuondokana na bajeti tegemezi kama Taifa na kuwa na Taifa lililoelimika lenye Utawala unaoheshimika. Katika hotuba yetu nimeonyesha wazi wazi kuwa tunazo fursa kubwa za kupata mapato ya ndani. Tatizo ni “MIND SET”. Changamoto kubwa tuliyonayo kama Taifa ni kwa viongozi kuwa tayari kujifunza kutoka kwa wengine bila kujali itikadi za kisiasa,ili kwa pamoja tuwaondolee umasikini Watanzania waliokalia raslimali zinazozidi mahitaji yao.Lazima sote tujiulize kwa nini wageni na wajanja wanatajirika,lakini wakulima na wafanyakazi wetu ni masikini? Taifa hili ni letu. Tusemezane, tujadiliane hatimae tusonge mbele.
Tuliyosema yanawezekena, yanahitaji viongozi na watumishi kuweka maslahi ya Taifa mbele. Raslimali tulizonazo zinatosheleza kama zitasimamiwa na kutumika kwa maslahi ya watu wetu.
Mheshimiwa Spika, naomba tena kukushukuru na kuwashukuru waheshimiwa Wabunge na Wananchi kwa kunisikiliza..
Mungu Ibariki Tanzania.
Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.
HAMAD RASHID MOHAMED (MB)
Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Msemaji Mkuu Wizara ya Fedha
Dodoma, 18.06.07
|
 |
 |
|
 |
 |
|
|
|
|