lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Historia ya Chama
»Kabla ya upinzani
»Chimbuko la Chama
»Kutambulishwa
»Mkutano Mkuu
»Usajili wa kudumu
»Kauli mbiu
b.part
Mengineyo
»Habari Mpya
»Makala mbalimbali
»Midahalo
»Blogu za wanachama
»Picha za matukio
»Maoni Yenu
b.part
Barua Pepe
jina la mtumiaji:
neno-siri
rt.bt.spc
bt.part2

Kuanzishwa kwa CHADEMA

Baada ya nchi ya Tanzania kutangaza rasmi kuwa nchi hii itaridhia kuanzishwa tena kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa, watu wachache makini waliona vyema kutumia fursa hiyo kwa ujasiri na kuanzisha vyama vya siasa vya kushindana kisiasa na chama tawala cha CCM. Ilikuwa kazi iliyohitaji ujasiri na kujituma sana. Ingawaje serikali ilitangaza kuwa iko tayari kwa kuanzishwa kwa mfumo huo, lakini ilidhihirika wazi kuwa serikali hiyo haikuwa tayari kuupokea kwa mikono miwili. Hii ilitokana na ukweli kuwa nchi yetu ina viongozi wengi waliokulia katika utamaduni wa kutokujua kuhojiwa au kukosolewa. Hata hivyo vyama vilianzishwa na moto wa mageuzi ukaanza kuwaka kidogo kidogo.

Kutokana na sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, ilibidi hata chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kusajiliwa upya. Katibu Mkuu wa CCM wakati huo akiitwa Horace Kolimba ndiye aliyekuwa Katibu Mkuu wa kwanza kuchukua hati ya usajili wa chama, na hili liliifanya CCM ijiite nambari wani kwa kuwa walichukua cheti wa kwanza na kwa kuwa walijipitishia wenyewe utaratibu kuwa CCM haikupaswa kuomba usajili kama vyama vyama vingine. Kati ya vyama vilivyoanzishwa ambavyo hadi kufikia uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 vilifikia jumla ya vyama 18 vilivyokwishasajiliwa, CHADEMA ndicho chama pekee ambacho Hayati Baba wa Taifa Mwl. Nyerere alitabiri kuwa kingeweza kuiritthi CCM katika kuongoza nchi na serikali.

CHADEMA ni kifupi cha maneno Chama cha Demokrasia na Maendeleo. Chama hiki kilianzishwa kwa bidii za waasisi wake chini ya baba wa chama Mhe. Edwin Mtei. Kama ilivyokuwa kwa vyama vingine, CHADEMA kabla ya kupata usajili ililazimika kufanya kazi ngumu. Viongozi waasisi wa CHADEMA walifanya kazi ya ujasiri ambayo ilikuwa ikitafsiriwa kuwa uhaini miaka michache tu iliyopita. Walisafiri jumla ya mikoa 22 kupata wanachama ili kutimiza moja ya sharti lililokuwa la aghali zaidi katika mchakato wa usajili. Kila walipoenda walipata mwiitikio. Lakini bado watu wengi wa Tanzania walikuwa wakidanganywa na kutiwa hofu kuwa siasa ya mfumo wa vyama vingi ni chachu ya mapigano na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

CHADEMA ilianzishwa kama jina lake lilivyo kwa makusudi ya kufungua uwanja mpana zaidi wa kukuza demokrasia na kuleta maendeleo katika nyanja zote za kijamii, kisiasa, kiuchumi kwa kusimamia yafuatayo:

  1. Kudaia mabadiliko makubwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ili kuwezesha kuondolewa kwa sheria zote kandamizi.
  2. Kuhakikisha kuwa watu wote wako sawa mbele ya sheria.
  3. Kusimamia kwa umakini utekelezaji wa mkataba wa haki za binadamu ambao nchi yetu iliusaini na kuuridhia mwaka 1948.
  4. Kuweka mazingira mazuri yatakayowawezesha wananchi kushiriki katika kukuza na kuumiliki uchumi.
  5. Kuweka msisitizo katika kukuza kilimo ambacho ni msingi muhimu wa uchumi wa taifa.
  6. Kuboresha huduma za jamii kama vile elimu, afya, maji na barabara hususani za vijijini.
  7. Kuweka kipaumbele katika uboreshaji wa miundombinu ya kiuchumi kama vile. mabarabara, reli, bandari na mawasiliano mengineyo.
  8. Kuachana kabisa na uendeshaji wa mashirika ya umma ya kibishara kwa kuwa mashirika ya serikali yalishindwa kuendesha shughuli za kibiashara kwa tija.
  9. Kuhakikisha kuwa kuna uwajibikaji katika huduma za jamii na uwazi katika mambo yote ya umma.
  10. Kuimarisha amani, utulivu na umoja wa kitaifa.
  11. Kulinda uhuru na kujenga umoja wa Afrika


...Inaendelea  Kutambulishwa kwa Umma
lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl