lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Historia ya Chama
»Kabla ya upinzani
»Chimbuko la Chama
»Kutambulishwa
»Mkutano Mkuu
»Usajili wa kudumu
»Kauli mbiu
b.part
Mengineyo
»Habari Mpya
»Makala mbalimbali
»Midahalo
»Blogu za wanachama
»Picha za matukio
»Maoni Yenu
b.part
Barua Pepe
jina la mtumiaji:
neno-siri
rt.bt.spc
bt.part2

Hali ya Tanzania kabla ya Vyama Vingi

Nusu ya pili ya miaka ya 1980 ilishuhudia ulimwengu ukiingia katika mabadiliko makubwa ya siasa ambamo nchi zilizokuwa zikiendeshwa kwa misingi isiyokuwa ya kuwashirikisha wananchi zililazimika kubadili mienendo ya mifumo yake ya siasa. Mifumo ya nchi nyingi hasa za Afrika ilikuwa ya kikiritimba sana. Nchi hizi ikiwepo Tanzania zilitumia mfumo wa siasa wa chama kimoja ambamo chama kilishika hatamu za uongozi wa nchi. Haikuwa rahisi kwa mtu yeyote kufanya siasa bila kujiunga na chama tawala. Hatua mbali mbali za maendeleo ya binafsi zilitegemea baraka za chama. Hii ni pamoja na kujiunga na vyuo vya elimu ya juu, kufanya biashara, kusafiri nje ya nchi na hata kupata ajira katika taasisi za serikali. Viwanda vyote, mashirika yote na taasisi zote vilikuwa na ofisi ya chama iliyokuwa ikisimamia uendeshaji na nidhamu kazini. Ofisi hii ilikuwa na nguvu kubwa kwani maamuzi yake yangeweza kuathiri hata maamuzi yote ya menejimenti.

Ikumbukwe kuwa Tanzania ilipata uhuru wake mwaka 1961 baada ya mapambano ya aina mbali mbali ambayo kwa pamoja yalizaa uhuru wa nchi hii. Ingawaje shughuli ya kupigania uhuru ilivishirikisha vyama zaidi ya kimoja lakini muda mfupi baada ya uhuru rais wa Jamhuri ya Tanganyika alitangaza kuanzishwa kwa mfumo wa siasa wa chama kimoja na kupiga marufuku uendeshaji wa chama chochote kingine cha siasa. Waliofurahia mfumo huo mpya na waliouchukia kwa pamoja walilazimika kukubali kuufuata na kuutii. Tangazo hili lilitolewa na TANU mwaka 1962 na nchi kuingizwa rasmi katika mfumo wa chama kimoja cha siasa kikatiba mwaka 1965.

Zipo sababu nyingi zilizosababisha viongozi wa Afrika wachague kufuata mfumo huu. Muhimu kati ya hizo ni kwa viongozi waliokuwa madarakani kujihakikishia usalama wao madarakani kwa muda mrefu watakavyo. Uchaguzi uliofanyika kati ya mwaka 1965 na 1990 ulijaa vibweka kwani kama mtu angelitaka kugombea nafasi yoyote angelazimika kujiunga na chama tawala ili aweze kugombea kwa kupitia chama hicho pekee nchini. Uchaguzi kwa ngazi ya urais uliwakutanisha rais na kivuli ambapo mpiga kura alitakiwa kuchagua ama mgombea mmoja tu aliyeko katika karatasi ya kupigia kura au kivuli.


...Inaendelea  Chimbuko la chama
lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl