8 Mei 2007
Hakuna uamuzi uliofanyika wa kusajili Chama kimoja
Si kweli kwamba vyama vinakutana kuanzisha chama kipya cha siasa. Ukweli ni kuwa viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani wamekuwa wanakutana kuendeleza majadiliano yaliyoanza toka mwanzoni mwa mwaka huu ya kutafakari kuhusu ushirikiano wa vyama vya siasa nchini.... |
|
21 Aprili 2007
Rai ya Vijana kwa Rais kuhusu suala la mikopo ya elimu ya juu
Mfumo wa uchangiaji uliopo hivi sasa unakinzana na Sera, Sheria na ilani ya Uchaguzi ya Chama kilichopo madarakani. Sera ya Elimu ya Juu ya Mwaka 1999 inazungumza kuhusu uchangiaji wa elimu kwa maana ya serikali kuwa na mchango wake na wananchi kuwa na mchango wake.... |
|
10 Aprili 2007
Bunge limchukulie hatua mbunge wa Mkuranga Malima
Mheshimiwa Spika, sina tatizo hata kidogo na haki ya Mheshimiwa Malima kukaidi uamuzi wako halali, bali kwa maoni yangu na kwa mujibu wa Katiba, Sheria na Kanuni zetu Mheshimiwa Malima ameingilia uhuru wa Bunge (Contempt of Parliament) na anahatarisha uhuru wa muhimili mmoja mkuu wa Dola, Bunge. Kwa maoni yangu, kitendo cha mheshismiwa Malima kulalamika kwa Katibu Mkuu wa CCM kwamba hakutendewa haki na Spika ni kinyume na Kanuni za Bunge, kanuni ya 4 (3)....
28 Januari 2007
Nyuma ya pazia la uchaguzi Tunduru
KWA mara ya kwanza, historia ya Tanzania imeandikwa upya baada ya idadi kubwa ya wananchi wa Wilaya ya Tunduru kuamua kutopiga kura katika uchaguzi mdogo wa ubunge uliofanyika Machi 18, mwaka huu chini ya ulinzi mkali wa polisi...
16 Januari 2007
Barua kwa Waziri Mkuu Edward Lowassa
Kama kweli wewe ulifahamau kuwa kuna mtu ametoa rushwa kwa wabunge na hakuchukua hatua zinazostahili kwa vyovyote vile ni kinyume na sheria, maadili ya uongozi na dhamira ya Mheshimiwa Rais Kikwete ya kupambana na rushwa bila kumfumbia macho yeyote.
Kwa upande mwingine tuhuma kwamba mhimili wa serikali (executive) unaingilia mhimili wa bunge (legislature) zinakuelekea wewe.... |
|
12 Januari 2007
Ndesamburo apongezwa kwa uamuzi wa kishujaa
Baada ya kutafakari sababu ulizozitoa tumeamua tukupongeze kwa uamuzi wako wa kishujaa wa kusimama bila ya hofu katika misingi ya haki, uadilifu na ukweli. Uamuzi wako ni ishara tosha kwamba wewe ni mbunge, kiongozi na mwanachama unayepeperusha vizuri bendera ya CHADEMA hususani katika kusimamia misingi yetu ya maadili, ukweli, demokrasia na maendeleo....
11 Januari 2007
Siogopi kufa, ili mradi niseme kweli - Ndesamburo
"Mwaka jana, Waziri Mkuu alimuita Mengi na kumwambia, usipoliondoa shauri utashindwa, Manji amewahonga wabunge wengi." Kutokana na sababu hizo, Ndesamburo jana alitangaza kujiuzulu ujumbe wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, akidai anajiengua kutokana na kashfa ya rushwa iliyoighubika..... |
|
11 Januari 2007
Eugen Maganga si Mkurugenzi CHADEMA
Ushauri wetu kwa vyama vinavyo andaa mikutano kwa ajili ya kupokea watu ni kwamba: Muajiri mwenye akili timamu hutafuta taarifa za kweli za mtu anayetaka kumwajiri. Vivyo hivyo ni vema vyama vya siasa vikajipa nafasi ya kupata taarifa za kweli za mtu wanaye mpokea ili akisimama jukwaani kutangaza historia yake wawe na uhakika wa anachokisema....
27 Disemba 2006
Ziara ya Mhe Freeman Mbowe Mwenyekiti wa CHADEMA Mikoani
Ndugu Watanzania, pamoja salam za heri ya Mwaka Mpya, kwa furaha kubwa tunapenda kuwajulisha kuwa Mhe. Freeman Aikael Mbowe Mwenyekiti wa Chama Taifa anatarajia kuanza ziara ya awamu ya kwanza ya mikoa kumi kuanzia kesho tarehe 28.12.2006 hadi tarehe 05.01.2007... |
|
5 Disemba 2006
Sakata la Mgogoro wa Ardhi Kawe
Mkutano wa wakazi wa Kawe B, jimbo la Kawe, Mkoa wa Dar es Salaam, uliofanyika tarehe 2, Disemba, 2006 katika viwanja vya shule ya msingi KaweB, uliingia dosari na hata kuvurugika baada ya Meya wa manispaa ya Kinondoni, Salum Londa kuonyesha ubabe na kumtisha Mwenyekiti wa kikao...
|