lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
»Habari Mpya
»Matamko ya Chama
»Makala mbalimbali
»Midahalo
»Blogu za wanachama
»Picha za matukio
»Maoni Yenu
»Katuni
b.part
Barua Pepe
   
jina la mtumiaji:
neno-siri
rt.bt.spc
bt.part2


15 Agosti 2007     
Hoja Binafsi ya kuunda kamati ya Bunge kumchunguza Waziri Karamagi
Mheshimiwa Spika, mapitio ya mikataba ya madini ni mchakato ambao mwisho wake ni kuletwa kwa sheria ya madini hapa bungeni na kuifanyia marekebisho ili kuiboresha na kuondoa mapungufu. Hivyo, mpaka hapo sheria itakaporekebishwa, ndipo tutasema tumemaliza zoezi la kupitia mikataba ya madini na hivyo kusaini mikataba mipya...

12 Agosti 2007     
Mkutano wa viongozi wa Vijana Afrika kufanyika Tanzania
Mkutano wa Viongozi wa Vijana wa Vyama Vya Kidemokrasia Afrika(DUA Youth Conference) unatarajiwa kufanyika Tanzania kuanzia tarehe 18 mpaka 20 Agosti 2007 chini ya CHADEMA kama mwenyeji. Mkutano huo wa siku tatu utajadili masuala ya maendeleo ya kiitikadi ya vyama vya kidemokrasia Afrika....

18 Julai 2007     
Hotuba ya Waziri Kivuli wa Mipango, Uchumi na Uwezeshaji Mhe. Z. Kabwe
Mheshimiwa Spika, ili kukua kwa uchumi kuwe na manufaa kwa Watanzania ni lazima serikali kwa makusudi kabisa iamue kuweka sera rafiki kwa masikini (pro-poor policy). Sera rafiki kwa watu masikini ni zile sera zinazoelekea kuweka rasilimali katika sekta zinazokua na zinazoajiri watu wengi zaidi. Kilimo ni sekta pekee inayoweza kuondoa umasikini nchini Tanzania....
9 Julai 2007     
Tanzania, CHADEMA, CCM na mjadala wa falsafa na itikadi Lipi ni jibu?
Tukikubali kufuata falsafa ya “nguvu ya umma”, tutaweza kuwawajibisha viongozi wetu kuweka sera zitakazohakikisha watanzania wananufaika na maliasili za nchi yetu kuliko wageni. Kama tutafuata itikadi ya mrengo wa kati tutaepukana na mzigo wa kuwa na serikali kubwa ambayo ni mzigo kwa walipa kodi. Tofauti na muundo wa kiserikali ya kijamaa ambao serikali kuu inakuwa pana yenye mikono kila mahali....
26 Juni 2007     
Uzoefu kuhusu Uendeshwaji wa Uchaguzi Tanzania
Kutokuwepo kwa sheria na utaratibu unaodhibiti matumizi ya raslimali wakati wa uchaguzi ulifanya pawe na utofauti mkubwa wa raslimali baina ya chama tawala ambacho kilikuwa kinatumia vyombo vya dola kutafuta raslimali na vyama vya upinzani kwa upande mwingine ambavyo vilikuwa vinadhibitiwa na dola kukusanya raslimali....
23 Juni 2007     
Ujumbe wa Vijana CHADEMA kuunga mkono BAVITA
Viijana na Watanzania wamengoja sana kuhusu baraza la vijana. Suala hili lilijiotokeza katika kikao cha bunge la Februari 2006 kutokana na swali la Mheshimiwa Halima Mdee, Mbunge wa Viti Maalum. Lakini majibu aliyoyatoa naibu waziri, Mheshimiwa Daniel Nswanzugwako bado yaliacha maswali na maswali mengine zaidi yamezuka kutokana na hotuba ya bajeti ya wizara....
2 Juni 2007     
CHADEMA imebeba Utume wa kizazi kipya
Tofauti na vyama vingine vya upinzani. CHADEMA ni tokeo la kukuwa kitaasisi na juhudi za wanachama wake katika kujiendeleza. Baadhi ya vyama vya upinzani viliibuka na kupata umaarufu miaka ya tisini kutokana na wanasiasa mbalimbali maarufu kuhama kutoka CCM na kujiunga na kambi ya upinzani...

29 Mei 2007     
Ni Rais Kikwete anayepaswa kuomba radhi!
Kutokana na ukweli kuwa wanaoathirika na mwenendo mbaya wa Rais Kikwete kufanya kampeni kwenye mikutano ya kiserikali ni watanzania kwa ujumla wao. Walio na vyama na wasio na vyama. Na kwakuwa kauli hizo za kikada ambazo zimethibitishwa na serikali kupitia waziri wa habari na utamaduni zilitolewa na Rais akiwa katika ngome ya CHADEMA....

14 Mei 2007     
TAKURU inalinda na kutetea Rushwa?
Rushwa ni kosa la jinai, rushwa ni adui wa haki. Kauli za kuwapa wala rushwa muda ama kukataa kuchunguza rushwa ni ishara ya kulinda uhalifu ambayo ni kinyume cha sheria kwa raia wa kawaida na hata taasisi za umma....
14 Mei 2007     
Sababu za Ushirikiano wa Vyama vya Siasa vya Upinzani
Mara nyingi suala la mashirikiano ya vyama limekuwa likizungumziwa pindi uchaguzi unapowadia au kwenye matukio maalum na hivyo kufanyika katika hali ya kurashiarashia na isiyokuwa ya umakini wa kutosha na hivyo kutofaulu malengo yetu....




endelea...     
lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl