lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
»Habari Mpya
»Matamko ya Chama
»Makala mbalimbali
»Midahalo
»Blogu za wanachama
»Picha za matukio
»Maoni Yenu
»Katuni
b.part
Barua Pepe
   
jina la mtumiaji:
neno-siri
rt.bt.spc
bt.part2


20 Februari 2008     
Vijana wa CHADEMA tunalaani vijana kukamatwa kuhusu JamboForum
Vijana wa CHADEMA tunaungana na wapenda uhuru, haki na ukweli kote nchini kulaani uamuzi wa Jeshi la Polisi kuwakamata na kuwaweka ndani vijana wa wawili wa kitanzania Maxence Melo na Mike Mushi kwa sababu ya masuala ya mtandao wa Jambo Forum...

19 Februari 2008     
Tume ya Uchaguzi inatumika kuhujumu CHADEMA Kiteto
Yamejitokeza matukio mbalimbali tangu kuzindua kampeni ambayo ni muhimu Umma ukaendelea kufahamishwa kwakuwa yanahusu tukio muhimu kwa mchakato wa Demokrasia na Maendeleo nchini...

2 Februari 2008     
Waraka wa kwanza kwa Wafanyakazi Vijana
Mwaka 2007 ulikuwa ni mwaka mzuri katika harakati zetu za kuhamasisha na kusimamia mabadiliko nchini. Kwa upande wa chama kwa ujumla ulikuwa ni mwaka ambao tulikuwa mstari wa mbele katika kupambana na ufisadi na kutetea rasilimali za Taifa...

28 Januari 2008     
Victor Kimesera kugombea ubunge jimbo la Kiteto
Kimesera amewahi kuwa mgombea katika jimbo hilo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 na kupata asilimia 42 ya kura zote wakati huo. Kimesera mwenye shahada ya falsafa amewahi kuwa mtendaji mkuu wa taasisi na makampuni mbalimbali ndani na nje ya Tanzania...

17 Januari 2008     
Waziri Magufuli ingilia kati hatma ya wakazi Kibamba
Kwa tamko hili naungana na wakazi wenzangu wa Jimbo la Ubungo wanaokaa katika Kata ya Kibamba kupinga kitendo cha kutaka kuwahamisha Kimabavu kutoka katika ardhi na makazi yao ambavyo wamemiliki kihalali kwa mujibu wa sheria za nchi ya Tanzania kwa kushirikisha ngazi zote za Serikali ya Muungano wa Tanzania...

10 Januari 2008     
Fisadi namba Moja, Daudi T.S. Ballali akamatwe!
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa, alimemtaka Kikwete kuamuru kukamatwa kwa Dalali na kuwekwa gerezani, hadi mahakama itakapotoa uamuzi kuhusu tuhuma za ubadhirifu wa fedha za serikali alizokutwa nazo....

7 Januari 2008     
Vijana CHADEMA tunalaani shambulio kwa Waandishi
Kwa niaba ya Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA), vijana wa CHADEMA tunaungana na wapenda haki na ukweli kote nchini kutoa pole kwa wanahabari Saed Kubenea na Ndimara Tegambwage kwa kushambuliwa kwa mapanga na tindikali...

8 Novemba 2007     
Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wamiminika CHADEMA
WANAFUNZI wa vyuo vikuu hapa nchini na wasomi wengine waliobobea ndio watakaoleta mabadiliko ya kisiasa na uchumi kwa kuwa jamii inawaamini kutokana na upeo wao wa kujua mambo na kuyachanganua bila kuburuzwa. Mbunge wa jimbo la Tarime, Chacha Wangwe alisema mjini hapa wakati wa kufungua tawi la vijana la chama cha demokrasia na maendeleo, CHADEMA linaloundwa na wanafunzi wa vyuo viwili mkoani humo...

6 Novemba 2007     
Tawi la CHADEMA Kawe lavunjwa kwa mara ya pili!
Leo asubuhi Novemba 6 mwaka 2007 Viongozi wa Vijana wa CHADEMA Jimbo la Kawe Manispaa ya Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam tulipokea taarifa ya kuvunjwa kwa mara ya pili Tawi la CHADEMA la “Ukombozi” lililoko katika eneo la Kawe Tanganyika Packers na bendera ya chama chetu kuteremshwa....

27 Oktoba 2007     
Ziara ya Dk. Slaa Marekani yaendelea kwa mafanikio
Katika ziara hiyo Dr Slaa amefanya pia Mkutano naizara ya Mambo ya Nchi za Nje (State Department) ya Marekani ambapo amekutana na Bwana Jeffrey R. Krilla, Naibu Katibu Msaidizi wa Idara ya Demokrasia, Haki za Binadamu na Kazi(Deputy Assistant Secretary, Department of Democracy, Human Rights and Labor) na Karen Gilbride - Mkuu wa Kitengo cha Afrika(Head Africa Section)...

10 Oktoba 2007     
Alichofanya Nazir Karamagi katika mkataba wa Buzwagi
Katika kipindi cha karibu mwaka mmoja ambao Mheshimiwa Karamagi ameshikilia madaraka yake ya sasa kama Waziri wa Nishari na Madini, amehujumu taifa la Tanzania kwa kusaini mkataba wa ujenzi wa Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi wilayani Kahama na kampuni ya Pangea Minerals Ltd ambayo ni kampuni tanzu ya Barrick Gold ya Canada....

27 Agosti 2007     
Maelezo ya Hoja ya kuundwa kwa kamati teule ya Bunge kuchunguza BoT
Taarifa nilizonazo zinajitosheleza kabisa kujenga hoja nzito ya kuliomba Bunge lako Tukufu likubali kuunda Kamati Teule ya Bunge. Taarifa hizi ni pamoja na Taarifa za uhakika kutoka vianzio rasmi kama vile BRELA, Federal Trust (MAURITIUS) Ltd ambayo ni Msajili wa Makampuni ya Offshore, ‘Registrar of Companies –Companies House, London’, Taarifa za uhakika kutoka ndani ya BOT...





endelea...     
lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl