MUNGU TUSAIDIE, MUNGU TUWEZESHE,
TANZANIA INA KILIO,
WANAO TWATESEKA MAOVU YANASHAMIRI,
NCHI YATEKETEA WATAWALA WANEEMEKA.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo,
Tumaini la ukombozi wa kiuchumi na kisiasa,
Chama cha Demokrasia na Maendeleo,
Chimbuko la fikra mpya nayo mikakati ya utumishi,
Mtetezi wa uhuru, uhuru wa kweli,
Maendeleo ya kweli wanayostahili Watanzania.
Mlinzi wa uzalendo raslimali za taifa la Tanzania,
Jukwaa la harakati kukomesha ufisadi, na uoza wa kimaadili.
KIITIKIO:
WanaCHADEMA tushikamane,
Demokrasia Yawezekana,
WanaCHADEMA tushikamane,
Maendeleo yawezekana,
Watanzania tushikamane,
Mabadiliko Yawezekana.
Wazee na akina Baba (twende),
Vijana na akina mama (amka),
Pamoja tuna umaskini (tuna maisha duni),
Pamoja tuna uchungu,
Watoto nanyi jiungeni (twende),
Tunaweza acheni(acheni) woga x 2
KIITIKIO:
WanaCHADEMA tushikamane,
Demokrasia Yawezekana,
WanaCHADEMA tushikamane,
Maendeleo yawezekana,
Watanzania tushikamane,
Mabadiliko Yawezekana
Nguvu ya Umma, People’s Power!
Nguvu ya Umma, People’s Power!