lf.bevel
MWANZO CHAMA SERA KATIBA TUUNGE MKONO UCHAGUZI TUWASILIANE
banner
Uzinduzi wa Chama
»Tumaini Jipya!
»Hotuba ya Uzinduzi
»Mpango Mkakati
»Marekebisho Katiba
»Bendera Mpya
»Wimbo wa Chama
»Kadi Mpya
b.part
Mengineyo
»Habari Mpya
»Makala mbalimbali
»Midahalo
»Blogu za wanachama
»Picha za matukio
»Maoni Yenu
b.part
Barua Pepe
jina la mtumiaji:
neno-siri
rt.bt.spc
bt.part2

Agosti 13, 2006, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA kilifanya uzinduzi mpya wa chama, uzinduzi ambao ulikuwa na lengo la kubainisha mikakati na Programmu mbalimbali za utekelezaji kuelekea uchaguzi ujao mwaka 2010, kwa lengo la kujipanga na kujijenga upya ili kuwaletea Watanzania Matumaini, Imani na Mwelekeo katika medani za uchumi, siasa na kijamii.

CHADEMA kilijipanga upya kwa maana ya kubadilisha mfumo na muundo wake, kilifanya mabadiliko ya katiba na kanuni ili viende sambamba na mahitaji na mazingira ya sasa ambapo CHADEMA imedhamiria kujipanua zaidi kuanzia ngazi ya msingi mpaka taifa.

Kwa upande mwingine CHADEMA kimeendelea kujipanga kuwa sauti ya wasio na sauti tuwatetea, kuendeleza na kutekeleza Mabadiliko ya Kweli na Uhuru wa Kweli. Chama kimedhamiria kusimamia uwajibikaji wa serikali na kuishinikiza kutekeleza ahadi ilizozitoa. Kitaendelea kuwa chenye mtizamo chanya na wenye kujenga katika kuiwajibisha serikali. Na kitakuwa na watu wa fikra, wenye nafsi wazi (open mind) na nishati katika kuibua mawazo na kutengeneza sera tunazohitaji kukabiliana na changamoto hususani za muda mrefu ambazo nchi yetu inakabiliana nazo. CHADEMA kinaendelea kuwa moja ya vyanzo vya imani, matumaini na mwelekeo wa Taifa letu.

Tunafanya hivi kujenga chama imara na makini zaidi ili kuongeza ufanisi katika ushindani demokrasia ya vyama vingi. Tunazindua mchakato wa kwanza unaohusisha zaidi mabadiliko ya kimuundo na zana kisha tutaanza mchakato wa maboresho ya kisera na uongozi. Tunazindua alama na zana sita za CHADEMA. Ndani ya alama na zana hizi upo ujumbe mahsusi kwa wanaCHADEMA na Watanzania. Alama na zana hizi ni ishara tu ya imani, matumaini na mwelekeo wetu kwa mustakabali wa chama na taifa letu. Tunatazama mbali, tukiwa na imani, matumaini na mwelekeo.

Miongoni mwa mambo yaliyozinduliwa ni pamoja na;

  1. Chama kuwa na bendera mpya na kadi mpya zenye rangi nne: bluu, nyekundu, nyeupe na Nyeusi.

  2. Uzundulizi rasmi wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa CHADEMA kuanzia 2006 mpaka 2010. Mpango huu umedhamiria kukiendesha na kukijenga kama “chama taasisi” na si “chama uchaguzi”.

  3. Mfumo na muundo mpya wa chama umejikita zaidi katika kuhakikisha na kutambua nguvu za makundi maalumu ya kijamii, kama vijana, wanawake, wazee na walemavu.

    Baraza la vijana linajulikana kama BAVICHA, yaani Baraza la vijana wa CHADEMA, Baraza la wanawake ni BAWACHA yaani na Baraza la wanawake wa CHADEMA.

  4. Wimbo rasmi wa chama utakaoimbwa kote nchini. Ni sauti ya CHADEMA. Ni njia ya kutumia sanaa kuwasilisha hisia, misimamo, hamasa, matamanio na matarajio yetu.

  5. Kauli mbiu ya uzinduzi mpya wa CHADEMA ni CHADEMA; TUMAINI JIPYA! Hii ni kauli mbiu inayobeba dhana nzima ya “imani, matumaini na mwelekeo”.


Tumaini jipya ni Imani, Ni matumaini, Ni mwelekeo!



lf.curl lf.curl2 rt.curl2 rt.curl