- TUMAINI JIPYA ni mchakato kuelekea 2010.
- Ni ujenzi mpya wenye kulenga harakati kuelekea uchaguzi wa 2010.
- Ni mwanzo na mwendelezo wa utekelezaji!
Tunataka CHADEMA kiwe chama cha namna gani kama matokeo ya uzinduzi wa TUMAINI JIPYA?
Tunataka CHADEMA kiwe sauti ya mabadiliko na matumaini kwa nchi yetu. Tutakuwa wenye mtazamo chanya na wenye kujenga katika kuiwajibisha serikali. Tutakuwa wabunifu katika kuibua mawazo na kutengeneza sera mbadala zinazohitajika kukabiliana na changamoto za muda mfupi na muda mrefu ambazo nchi yetu inakabiliana nazo.
Tunaamini kuwa changamoto hizi ni tata na zinazoingiliana ambazo kimsingi zinahitaji tafakari makini na ya kina. Lakini tunapata moyo na kuamini kuwa yote yanawezekana kwa kutumia misingi ya falsafa yetu ya Nguvu na Mamlaka ya Umma. Tunaamini kuwa kwa kutumua falsafa hii tutaweza kuendeleza sera na mawazo yenye kutimiza matarajio ya Tanzania na watu wake katika karne hii ya ishirini na moja.
Katika siasa mwelekeo ni kitu muhimu sana, kwahiyo uongozi wa sasa wa CHADEMA unatoa mwelekeo bayana wenye malengo! Ni mrindimo wa mawazo ambao unaweza kujibu hatua muhimu kwa mafanikio ya CHADEMA, na hatimaye ukombozi wa taifa hili.
Tunaamini, na tunawaomba watanzania waamini kuwa, CHADEMA iliyozinduliwa upya, chini ya Uongozi thabiti wa Freeman Mbowe inayofursa nzuri ya kutoka katika kushindwa na kujizatiti kwa ajili ya ushindi. Na pindi kitakaposhinda, CHADEMA kinayo fursa ya kuibadili nchi hii kuelekea katika hali bora zaidi. Na humo ndimo ilimojikita falsafa ya uzinduzi mpya! TUMAINI JIPYA!
Tunaamini kuwa CHADEMA inao wajibu wa kujenga chama imara na baadaye taifa lenye nguvu za kiuchumi, kisiasa na ushawishi mkubwa kwa kutumia maliasili na watu! Watu waliojaa uungwana na upendo uliotukuka, upendo ambao haupatikani kwa taifa jingine isipokuwa Tanzania, Uungwana ambao kimsingi ndio msingi wa amani yetu.
Upendo na Ukarimu ni bidhaa adimu sana ambayo nchi yetu imejaaliwa kuwa nayo, kimsingi ni rasilimali muhimu sana ambayo ni taifa letu pekee limejaaliwa nayo…
Upendo na uungwana ni rasilimali muhimu kwa ukuaji wa uchumi na maendeleo ya watu kwani vinatoa fursa kwa serikali iliyopo madarakani kujenga uchumi na kutoa huduma muhimu za kijamii.
Tunaamini kuwa pindi CHADEMA kitakapopewa uongozi wa Taifa hili, kitaweza kutafsiri upendo na uungwana wa watu wa nchi hii katika mantiki za uchumi imara, huduma bora na zaidi kulifanya taifa letu kuwa na ushawishi mkubwa duniani. Tunaamini kwa kutumia rasilimali amani upendo , CHADEMA Itajenga taifa lenye Uhuru kamili!.
CHADEMA tunamuomba kila Mtanzania aamini kuwa mabadiliko yanawezekana, na kwamba ili yawezekane ni lazima yaanzie kwake, kila mmoja akiamini hivyo, ukombozi unawezekana.
Tuunge mkono sasa!, tuunge mkono leo!, jiunge na CHADEMA leo! CHADEMA kinamjali kila Mtanzania, kinasimamia haki, kinasimama kwa ajili ya wote. Ni chama chenye dira na ni chama chenye mwelekeo. Kinatoa fursa kwa wote, kina mawazo mapya kina mawazo mbadala , na zaidi kinawakilisha mtu kama wewe!
CHADEMA; Mabadiliko ya kweli, Uhuru wa kweli.