Uzinduzi mpya wa chama hapo Agosti 13 2006 uliambatana na uzinduzi wa kadi mpya za uanachama wa CHADEMA.
Tumeamua kuleta imani, matumaini na mwelekeo zaidi katika uanachama na sasa tutaanza kuandikisha wanachama upya. Tumeamua kusitisha utamaduni wa kutoa kadi bure ingawa kadi za CHADEMA bado zitaendelea kuuzwa kwa bei ndogo ili kila Mtanzania aweze kugharamia.
Lengo ni kuhakikisha kila anayechukua kadi ya chama anachangia kama ishara ya nia yake ya kuunga mkono chama na harakati za ukombozi wa nchi hii. Tunataka tuwe na wanachama hai chini ya mkakati wa “CHADEMA ni msingi”. Tunataka wanachama wamiliki na kukiendesha chama. Michango hii midogo midogo ikiunganishwa pamoja ni nguvu ya pekee katika kuchochea kujitegemea na kuendesha chama kwa nguvu ya wanachama. Kama ambavyo bahari ni muunganiko wa matone madogo madogo ya maji ndivyo ambavyo michango hii inaweza kukijenga chama. Tunataka uanachama uwe chachu ya imani, matumaini na mwelekeo wa CHADEMA.
dokezo: