Uchaguzi wa Afrika Mashariki - Demokrasia yabakwa
Leo Bunge la Tanzania lilitakiwa kuchagua wawakilishi wake katika Baraza la kutunga sheria la Afrika Mashariki (East African Legilstative Assembly). Uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za Bunge la Tanzania, Mkataba wa Afrika Mashariki na kanuni ndogo za uteuzi wa Wabunge wa Afrika Mashariki. Leo tumeshuhudia, kwa mara nyingine tena, CCM wakitumia wingi wao ndani ya Bunge kuminya demokrasia na kukanyaga bila woga maslahi ya nchi yetu.
Kanuni za Bunge na Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zinataka uwakilishi uzingatie uwiano wa vyama ndani ya Bunge.
Kambi ya upinzani ilitengewa nafasi moja tu licha kuongeza viti vyake kutoka 17 mwaka 2001 mpaka 45 mwaka 2006. Na hata hako ka nafasi kamoja ka upinzani CCM wameamua kuwachagulia kwa kumpa kura Mzee Msha ili kumpa zawadi John Cheyo ambae siku hizi anaimba nyimbo za CCM. Nikikumbuka kuwa Cheyo ndie mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali (PAC), machozi yananitoka kwani sasa serikali itaponda mali ya umma itakavyo maana hakuna chombo ya kuizuia. Cheyo ameshapewa carrot!
Katika Bunge la Afrika Mashriki kuna nafasi tatu kutoka Zanzibar. Kanuni inasema uwiano wa vyama. Zanzibar CUF na CCM zipo neck to neck. Lakini nafasi zote za Zanzibar zimechukuliwa na CCM. Maslahi ya Zanzibar katika Afrika Mashariki yapo mashakani.
Kiongozi wa Upinzani Bungeni anaomba mwongozo wa Spika ndani ya Bunge, Spika anafoka na kutishia. Haki imaminywa.
Niliamua kutoka nje ya Bunge na kususia uchaguzi. nikiungana mkono na wabunge 4 wa CHADEMA na wabunge wote wa CUF. Wabunge mashujaa wa CHADEMA waliotoka ni Bi. Halima Mdee, Bibi Maulidah Anna Komu na Chacha Zakayo Wangwe.
Kwa nini nimewalk out? Ni kwa sababu ya Principle - Misimamo isiyoyumba.
Mimi niliamua kuwa mtu wa principles mara tu niliamua kuanza siasa.
Nilitoka nje ya Bunge kwa sababu sikutaka kuingia katika histroia ya kukanyaga demokrasia. Ninaamini uchaguzi huu ni batili kwa sababu kanuni za Uchgauzi hazikufuatwa toka mwanzo wa mchakato.
Siamini katika CCM kutuchgaulia wapinzani Mbunge wake.
Siwezi kuramba miguu ya CCM, chama ambacho asilimia 90 ya wabunge wake wameingia Bungeni kwa takrima (soma rushwa). Walk out, ni kuonesha kuwa siridhiki na mchakato wa uchaguzi. Sikubaliani na kuburuzwa.
Ninawajutia Watanzania. kuamua kuchagua Bunge lililojaa chama kimoja. Hawapati thamani ya kura zao.
Najiuliza. Katika hali kama hii ya demokrasia ndani ya Bunge. Kuna haja ya kuwa Mbunge? Sipati Jibu. Nachanganyikiwa.
Je, hakuna njia nyingine ya kuimarisha demokrasia katika nchi? Demokrasia ya vyama vingi. Natafuta kitabu kinachoitwa 'ending one party dominance: Doroth Solinger. yeyote atakayepata kitabu hiki popote pale, anifanyie utaratibu nikipate. Labda nitapata mikakati ya kuimarisha demokrasia ya vyama vingi nchini.
Ni kupitia Bunge lenye angalau theluthi ya Wabunge kutoka upinzani, ndio Watanzania watapata thamani ya kura na kodi wanazolipa. Vinginevyo, nikitumia msemo wa Freeman Mbowe Bunge litabaki kuwa mchezo wa kuigiza katika Luninga (rejea makala za Freeman Mbowe za mwaka 2003).
Natoa wito kwa vijana wa Tanzania mliopo popote duniani, tuungane kuimarisha demokrasia nchini petu. This is a noble call. Wale wanaoweza kushika majimbo na waseme mapema ili tuyaandae majimbo yao, wale wasioweza wachangie mawazo na rasilimali ili kuweka miundombinu ya demokrasia katika nchi yetu. Muundombinu mkubwa ni vyama imara vya siasa vyenye mtandao mpana na sera za uhakika na zinazotekelezeka. Inawezekana, timiza wajibu wako katika ujenzi wa demokrasia.

11 Comments:
Juzi niliandika kwa hasira kidogo. hata sikusema kwa nini uchaguzi wa Afrika Mashariki ni batili. Uchaguzi huu uligubikwa na matatizo yafuatayo
1. Kanuni za uchaguzi hazikufuatwa. Licha ya kutoa taarifa kwa Katibu wa Bunge tangu tarehe 1 sept 2006 kuhusu kuboresha kanuni, hakuna hatua zilizochukuliwa. Kanuni ya kwanza iliyovunjwa ni kanuni namba 13 inayotaka katibu wa Bunge kuwasiliana na vyama - ambapo kwa mujibu wa kanuni za Bunge vyama ni kambi za vyama. Katibu wa Bunge aliamua kuandikia vyama vya siasa barua. Lengo ni kuvigawa vyama na hivyo kutokuwa na mgombea mmoja ili CCM ichague mgombea inayemtaka.
2. Mwaka 2001 wakati uchaguzi wa Wabunge wa Afrika mashariki unafanyika, kulikuwa na wabunge 17 tu wa upinzani. Leo Bunge lina wabunge 45 wa upinzani. Tuliomba nafasi ya Upinzani iongezeke mpaka 2, Katibu wa Bunge hakujibu na kusingizia kanuni.Kanuni za Bunge hazitaji idadi ya wabunge kutoka upinzani wala chama tawala, isipokuwa inataja makundi tu ya kugombea.
3.Kati ya Wabunge 65 wanaotoka Zanzibar katika Bunge la Muungano, wabunge 25 ni wa CUF. Hii ni takriban asilimia 40. Hivyo tukasema katika nafasi tatu kutoka Zanzibar, angalau moja itoke chama cha CUF. Katibu wa Bunge akagoma. Hakujibu hoja hata moja. Wanasingizia kanuni. Kanuni hazitaji idadi ya nafasi kwa makundi. Idadi inawekwa na Spika. Hivyo, ilikuwa ndani ya Uwezo. CCM wakamwekea ngumu Spika. Spika, ambae hivi karibuni amesifika kwa kuliimarisha Bunge, akasalimu amri.
Kambi ya Upinzani imeamua kwenda Mahakamani. Mahakama itasema kama kanuni zilikuwa sahihi au hapana. Haki itatendeka katika kujenga demokrasia.
9:52 PM
Leo nimesikia kupitia kwa Dr. Willibrod Slaa,Katibu Mkuu wa CHADEMA kuwa Spika wa Bunge amenitaka niombe radhi kwa kusema kuwa ama hajui kanuni au anapindisha kanuni ili kusaidia Chama cha Mapinduzi. Nimepewa mpaka tarehe 11 nov kuomba radhi. Kwanza siji ni kwa nini Spika wetu Mhe. Samwel John Sitta anaanza kufuata nyayo zile zile za Spika aliyemtangulia. Bunge linaanza kugeuzwa mahakama.
Spika Sitta tangu ameiingia katika kiti amekuwa mstari wa mbele sana kuliimarisha Bunge kama asasi. Katika hili nimekuwa nikimuunga mkono na kumpa moyo sana kwani ndio legacy yake.
Sitta amekuwa akipigwa vita na baadhi ya wabunge wa CCM kiasi cha kuanza kufikiria kumtoa katika nafsi yake. Mimi niliwasikia wabunge wa CCM kwa masikio yangu na ninaweza kuwataja kwa majina wakilalamika kwamba Spika anapendela wapinzani na kwamba inabidi wamtoe. Waziri Mkuu amekuwa akilalama chini chini juu ya Spika kwamba analipa nguvu Bunge ili kumdhibiti yeye. Na hivi sasa Waziri Mkuu amepanga timu ya wabunge kupinga mabadiliko ya kanuni za Bunge ambazo Sitta anataka ziboreshwe.
Sitta ni mwanasheria mahiri. Amekaa nje ya Bunge kwa Miaka kumi na hivyo akaja na mawazo mazuri sana ya kuliboresha Bunge. Mimi nimekuwa miongoni mwa wabunge wa mbele kabisa katika kuhakikisha nia ya Spika kuimarisha Bunge inatimia. Mimi nitakuwa wa mwisho kumyundermine. Spika anajua ananipenda sana na amekuwa akinipa moyo sana katika kazi zangu za ubunge. Mimi namwona kama njia ya kuimarisha demokrasia nchini kwetu.
Lakini juzi Spika amevunja kanuni za Bunge. Mimi sio mnafiki. Nitasema hili mbele yake.Kwamba amevunja kanuni ama bila kujua au kwa makusudi. Hili la bila kujua kwangu lina uzito mdogo. Hili la pili la makusudi ni kubwa zaidi. Amevunja kanuni ili kuridhisha chama chake ambacho yeye ni mjumbe wa Kamati Kuu. Spika Sitta, alikuwa akijua kuwa anavunja kanuni. Mimi namjua. Nilivyomwona anavyoongea, na alponikatalia kuongea na kuomba ufafanuzi nikajua hapa Spika anavunja kanuni makusudi. CCM wanambana Spika. CCM wanatuharibia Spika wetu. Spika ambae ni tegemeo la wabunge na wananchi ili kuifanya serikali ifanye kazi. Watu walienda kumshtaki kwa Rais kuwa anaibana sana serikali. Waziri Mkuu Lowasa ndie alifanya hivyo. Najua. Spika sasa ile kasi na viwango inamwishia. Namwambia Spika, asitishwe na hao wahafidhina wa CCM wasiotaka mabadiliko. Umefanya mabadiliko makubwa TIC, ni lazima ufanye mabadiliko ya Bunge. Historia itakuandika vizuri. Achana na vitisho vya kina Lowassa wasiopenda demokrasia ishamiri. Najua wewe ni muumini wa demokrasia.
Spika aliamua kuvunja kanuni ili kusaidia chama chake. Huu ndio msimamo wangu. Sitabadilika.
7:42 PM
Naunga mkono hoja ya kutobadilika. Nitatoa maoni yangu kuhusu masuala mengine uliyoyadokeza siku za usoni
5:50 PM
Naunga mkono hoja ya kutobadilika. Nitatoa maoni yangu kuhusu masuala mengine uliyoyadokeza siku za usoni
5:51 PM
Ndugu yangu Zitto, mimi nakuaminia. Sikupi pole; nakupa hongera kwa kuweza kusimamia ukweli. Uliyoyaongea kuhusu speaker kwa waandishi wa habari naamini ni ukweli ambao wengi wanajua hivyo. Tofauti yako na wengine ni kwamba wewe umekwenda mbele na kuusema huo ukweli hadharani, wengine ama wamekaa kimya au wameongea na wake/waume zao tu basi. Hii ndio kasumba yetu na inazidi kututafuna mpaka wakenya watakapokuja kututawala ndani ya EAC. Kwetu mkubwa haambiwa amejamba! Ulichofanya wewe ni kuvunja huu mwiko na kumwambia Sitta kuwa kajamba, tena kajamba kijambo chenye harufu kali na mbaya sana badala ya kumwambia etu upepo wa shetani umepita!
Siungi mkono kuomba radhi kiutu uzima kama alivyopendekeza moja ya wachangiaji kule TEF. Ufanye hivyo tu kama uliyoyaongea ama si ya kweli au huna uhakika kama ni ya kweli. Kama una uhakika shikilia msimamo wako. Nenda mbele zaidi uandkike mawazo yako jinsi unavyoona Sitta kavunja kanuni ukidorosa vipengele muhimu vya katiba,kisheria na kanuni za bunge letu na mabunge mengine katika jumuiya ya madola. Itabidi ukae na wanasheria wazalendo hasa Tundu ili mpitie sentensi baada ya sentensi na neno baada ya neno katika statement utakayoandika.
Katika kuisoma hiyo statement bungeni, uwe umetulia tuli usiwe na wasiwasi; all the time ukisoma hiyo statement umwangilie speaker Sitta straight on his eyes.
Ndugu yangu Zitto ukiomba msamaha, kuna hatari ya kushusha hadhi sana ubunge wako. Kumbuka hii itakuwa mara ya pili kuomba msamaha katika kipindi kisichozidi mwaka tangu uingie bungeni. Hii haitatoa picha nzuri kwa wapiga kura wako. Utaonekana wewe ni mwongo! Hamna kitu kibaya kwa mwanasiasa kama kuonekana kwamba ni muongo hasa kwa wapiga kura wake!
Bora wakupe adhabu uitumikie kwa kusema ukweli kulikoni kuomba msamaha huku ukijua kabisa humaanishi katika huo msamaha (yaani msamaha wa kinafiki). Hapa ndipo pa kuonesha tofauti katika ya wanasiasa wazee na vijana kwa upande mmoja, na wanasiasa wa CCM na upinzani kwa upande mwingine.
Chama pia lazima kikusaidie katika hili. Kwa jambo kubwa ambalo uliliongea sidhani kwamba uliongea 100% as an individual. You spoke as an institution, first as an MP and second as CHADEMA and opposition. Our party and other opposition parties must stand on your side. I will be staggered if the CHADEMA leadership will stand back and just witness your crucification without any empathetic and sympathetic support.
Mwisho: najua utatishwa sana. Lakini utambue kuwa hizo ndizo gharama za kuwa mpinzani katika nchi zetu za kiafrika zinazoongozwa na miungu watu. You have started the race, keep up the struggle. Unfortunately, some of us have no much help other than writing in this kind of forum sympathetically.
Best wishes in your struggle to give our politics a new look.
9:39 PM
big up sana
12:49 PM
Hapa ndipo ninapoishiwa-ga nguvu na utamaduni wetu waafrika.."kumwambia mkubwa wako ukweli huonekana ni kama huna adabu, na ni lazima uombe msamaha" hivi mabadiliko yatakuja vipi bila kuambiana ukweli? Kwa mtazamo wangu kabla hujamuomba msamaha, muombe nafasi umuelezee kile unachokijua katika hizo kanuni za uchaguzi(kwa vithibitisho vya rejea), halafu elezea ulichokiona anaenda kinyume nacho (kwa mifano halisi) baada ya hapo sasa ndipo utoe msimamo wako kwamba umeona kwamba hafuati zile kanuni na ndiyo maana ukasema "ama hajui ama anapindisha.." sasa atakavyopokea hoja yako ndipo utajua kama wewe uombe msamaha au yeye( hivi mzazi kweli hawezi kumuomba msamaha mwanae?)
Kuleta mabadiliko kunahitaji moyo ndugu yangu kaza buti tuko sambamba na wewe lakini pale tu utakaposema ukweli.
3:12 PM
This post has been removed by a blog administrator.
5:36 PM
Of course, demokrasia Tanzania haipo. Si tu kwamba haipo, bali pia watendaji wa Idara kuu za serikali kama vile Utendaji (Excutive branch), Bunge (legislative branch), na Mahakama (Judicial branch) hawajui wanachokifanya.
Inasikikitisha sana kuona spika wa bunge akifanya kazi za mahakama ndani ya bunge badala ya kutekeleza wajibu wake.
Nakubaliana na Kabwe kuwa inabidi watanzania walioko ndani na nje ya nchi washirikiane ipasavyo ili kubadili sura ya bunge la sasa ambalo linatawalia na chama kimoja. Hii haitawezekana bila kuanzishwa kwa grass-root movements, ambazo zitawabana wabunge wanaochaguliwa kuwajibika kwa ajiri yao.
Lakini zaidi ya hilo, vyama vya upinzani navyo vinapaswa vijipange vizuri. Sera za kueleweka zinatakiwa kuwekwa mahala pake kama kweli tunataka demokrasia ya kweli ishamiri nchini. Kuna makala nzuri sana hapa inayoelezea kuhusu mapungufu ya vyama vya mageuzi nchini. Soma ukipata muda: http://www.bongotz.com/bongoyetu17.html
5:41 PM
kijana njoo room kwangu uone picha zako
10:59 AM
hi
1:16 AM
Post a Comment
<< Home