Karibu katika blogu yangu
Ndugu zangu, washkaji zangu, wanaharakati wenzangu na wanasiasa wenzangu,karibuni sana katika blogu yangu. Nimechelewa sana kuanza kuandika kwa sababu ya uzembe kwa kweli. Nirahisi sana kusema kuwa majukumu ni mengi, lakini hiyo ni excuse tu.
Nitakuwa nina wajulisha mawazo yangu juu ya masuala mbalimbali. Nami pia ningependa kupata mawazo yenu.
Asanteni sana
"Mabadiliko ya kweli, Uhuru wa kweli"

18 Comments:
Hapo kale palitokea mnyama mmoja ambaye alikuwa na njaa sana na njaa ilipomzidi alijikuta akila hata mavi yake kuogopa kifo cha njaa,japokuwa mnyama huyo alichaguliwa kuwa kiongozi wa wanyama wengine kwani walimuamini kuwa anaweza kuwatetea hata nchi za mbali na kupewa msaada wa chakula kwa ajili ya wanyama wenzake.siku moja akawa amesimamia msimamo wake kuwa yeye ni mtetezi wa wanyonge ila hakuwa tayari kufa njaa mara alipotishiwa ya kuwa huenda akakikosa chakula alisitisha msimamo wake na wakati akiwa ameutangazia umma wa wanyama kuhusu hilo wanyama wengine walimshauri kuwa ni bora akawa na msimamo wa awali kwani ndio msimamo wa wale wanyama wengine naye akakubali je?huyo ni mnyama mwenye msimamo ama anaangalia asife njaa?huyu ni zitto kabwe na msimamo wake wa kuomba radhi spika yeye anataka aonekane kuwa ni mtu mwema mbele ya spika na pia jamii imuone kama mtetezi wao ndugu zitto tamaa ya chakula cha siku moja isikuyumbishe kiasi hicho.acha kutudhalilisha vijana wenzio kwani spika alikutukana kuwa wewe ni fedhuli,mkaidi na kuwa ujana wako ndio unakufanya ushindwe kuamua na kwa kweli utoto wako nimeanza kuuona kwenye website ya kumekucha kwani maelezo yako hayana mantic yeyote kumbe huwezi kuwa na msimamo ila unafuata maneno ya watu kila unachofanya unawataka watu wakuambie kweli hiyo ni aibu mbele ya TAIFA HILI.acha kujipendekeza wewe na ningekuwa chadema ukweli ningehakikisha walau wanakupa adabu ama ufukuzwe chama kwani kuna faida gani ya kuwa na mbunge anayejidhalilisha mbele ya umma eti kwa sababu tu spika ni rafiki yake awe tayari kuwatosa wabunge wote aliotoka nao nje bungeni?acha umalaya wa kisiasa wewe usifikiri unapendwa na hao CCM ama kajiunge nao basi kwani unakoelekea sio.naomba niishie hapo kwani presha yangu imenipanda sana na kwa hiyo nitawasiliana na wewe baadae,ila umalaya wa kisiasa acha.
7:07 PM
zitto wewe ni miongoni mwa watu ambao hamna msimamo kabisa na ni aibu kwa mtu kama wewe kuweka kwenye website eti unaomba umma ukupe mawazo wacha hiyo aibu na itakumaliza kisiasa ama kama umeamua kujiunga na ccm basi tuambie ili tujue moja.
7:11 PM
may GOD bless you in your politics but dont play with our problems for your interests.we are saying this to u and please if you nhave an e mail for mr.mbowe tell and i will say to him the kind of boys he do trust in chadema so tha he will be able to know whom he is accompanied with.
7:14 PM
kwa mlalahoi,
sikiliza mlala hoi comments zako kwa mh zitto zinatuchafua,alichosema ni kuwa amefungua shauri mahakamani kuangalia uhalali wa uchaguzi jinsi ulivyo endeshwa ,hiyo ni hatua ya kupongezwa.pili anachoomba radhi ni kile kitendo cha kuongea nje ya bunge,hasa ukizingatia zitto na sitta ni watu walio na mahusiano mazuri,kwa namna moja au nyingine zitto anaweka akiba kwa mzee huyo hiyo ni busara.
mambo ya siasa kwakuwa ni safari ndefu hayataki jaziba.msimamo wa zitto uko palepele na ndio maana kuna shauri mahakani,issue ingekuwepo kama angesema naomba radhi na ni na futa shauri mahakamani,kauli kwamba ni malaya wa kisiasa sio nzuri
1:10 PM
Kijana Pole na majukumu yanayokubana.
Nimeona maelezo ya wengine mengine kuhusu msimamo wako. Suala la muhimu ni kuwa na msimamo tu kujua unafanya nini kwa sababu gani. Hasa kwa kukumbuka wananchi wako ulivyo ahidi wakati wa Kampeni. Nakutakia Msimamo thabiti.
Kieza
6:21 PM
Hi Zitto,
Wewe umekuwa ni kioo cha wanaharakati vijana hapa Tanzania.
Uwezo wako wa kujieleza na msimamo wako dhabiti ndani ya bunge ni vitu adimu kwa vijana wengi wa rika lako.
Mimi ni kijana mwenzako na kwa kweli nimevutiwa sana na siasa hasa baada ya kuona sura za viana kama wewe mkifanya mambo mazito na yenye maana katika nchi yetu.
Nakutakia maisha marefu na mema katika mapambano ya kuwakomboa wanyonge na hatimaye ipo siku wanyonge watakuwa huru katika Taifa lao.
Keep up Zitto.
Erasto C. Mbalafu
0787-008201
Dsm
5:08 PM
MR.ZITTO
Nashukuru kuona kuwa umeweza kuwaweka roho juu wale ambo wameshika majukumu ya serikali kwa nia mbaya na hawaelewi wakifanyacho na hawapaswi kuwa hapo walipo hasa pale bungeni.
sasa naamini yakuwa niwakati muafaka wa kukumbushia mambo yaliokuwa yamejificha hasa ubadhilifu wa mali ya umma unaofanywa na baadhi ya vigogo.
Pili naomba sana uwe na e-mail au number ya simu ambayo kwa muda fulani uwe maalum kwa kupokea maoni na malalamiko ya watu moja kwa moja ili uweze kuwapa uwelekeo ulio sahihi, kwani ninachoamini mimi ni kwamba wewe;naomba nitumie kimombo kidogo kwani sina neno la kiswahili hapa:NI"USER FRIEND"
NI MIMI MPENDA MAENDELEO
KOMBA.A.M
1:34 PM
Big up Zito,wewe ni mfano wa kuigwa kwa vijana wa kitanzania.Lakini ndugu yangu nakuasa usije ukawa kama Tambwe,Ngawaiya,Kaburu na wengine wa aina hiyo hata siku moja maana hufanani nao hata kwa muonekano tuu. Ukifanya hivyo LAANA NA IWE JUU YA KICHWA CHAKO DAIMA KWA USALITI.
9:03 PM
Nina hadithi moja. Kuna bwana mmoja alipata ajali.Kulitokea vijana wakahangaika kumtoa yule bwana ndani ya gari lakini huku wanamsachi hela mifukoni, wakamchukua na kumtia kwenye gari lengine ili apelekwe hospitali. Kulikuwa pia na watu wengine ambao wao walikuwa wanajiona wastaarabu au tuseme waungwana kwa vigezo vyao ambao wao walikuwa wamesimama pembeni na kuangalia tu huku wakisema kuwa hawa vijana wabaya sana wanajifanya kumsaidia huku wanamuibia. Lakini wao walikuwa wanaanagalia tu bila ya kusaidia lolote. Dhamira ya ndani kabisa juu ya harakati hizi unazofanya unazo wewe mwenyewe, sisi tunaangalia unachofanya sasahivi. Wewe ni miongoni mwa vijana wachache sana ambao taifa hili limebahatika. Utakachofanya kama ukipewa madaraka hiyo siyo issue sasa hivi lakini kubwa ambalo lipo sasa ni ufisadi uliopo ndani ya serikali yetu. Wewe pamoja na wanasiasa na wanaharakati wengine mnadiriki kusema na kuanika, watanzania tuone na tuchukue hatua.
12:25 PM
mh Zitto..
mie sina chama maalumu ni mpenda haki,na mpenda wa chama kimoja, chama cha Tanzania.
Nakupongeza sana kwa hatua ya kuweka blogue hii na kuweza kuwasiliana na wananchi kwa ujumla,ina onyesha jinsi gani unavyoenda na wakati na hivyo kwangu mimi pia ni kipimo cha uwezo wako wa kufikiri lakini zaidi inaonyesha jinsi ulivyo mwakilishi na sio tu mbunge jina.
Ndugu mh nina kuunga mkono na misimamo yako na I pray to God to give you the strenght to fight for the rights of your people.
Mie nipo masomoni nchini India na inaniuma nikilinganisha kasi ya maendeleo nchini humu na nchi yangu.
Waindi hupenda nchi yao sana na viongozi nchini humu huchaguliwa kwa kuzingatia hayo na sio chama.
Kwa watanzania tulio India tunapata tabu kujibu maswali mengi.Maana ukikutana na muhindi maswali ni kama yafuatayo.(in order).
la kwanza:
native country(akimaaanisha nchi uliyotoka) saa ngingine kwa Indian English anasema from which country.
la pili:
anauliza Tanzanian currency how many Indian Rupees..anataka kujua thamani ya pesa ya nchini kwetu kulingana na kwake...
la tatu:
Arent there colleges in your country..akitaka kujua kwa nini umekuja kusoma India na sio nchini kwako,wengi wetu hudanganya kwa kusema twataka kujua Indian culture..
hayo maswali ni mazito sana kwetu..
Na ukiyatafakari vizuri utajifunza vitu vingi kuhusu muhindi na nchi yake na personality yake kwa ujumla.
Mie najifunza mengi baadhi yake ni yafuatayo:
kutoka swali la kwanza:
Kitambulisho cha mtu ni nchi yake na sio jina lake kama wengi wetu wanavyodhani..
Swali la pili:
Muhindi hupenda pesa..(he he hapana sio hilo tu)
Muhindi anataka kujua nchi yake inasimama wapi katika ramani ya dunia...na pesa kwake ndio uchumi na kilinganishi cha kidunia cha thamani ya nchi yake...
La tatu:
Ana amini kuwa kila kitu kinaweza kupatikana nchini mwake na kama hakipo atajaribu kufanya kiwepo..
Na hushangaa wale ambao washindwa kukipata nchini mwao..
Nakutakia kila la heri mh Zitto Kabwe.
9:45 AM
Mh Zitto,first congratulations for the hard job of working for your people,what i mean is uongozi ama ubunge ni mzigo mzito na si privelage peke yake ndio maana viongozi hawawatumikii wananchi badala yake wananchi ndio wanawatumikia viongozi.
Ni kweli kenye historia ya Tanzania kumekuwepo pepo za kisiasa tofauti tofauti kuanzia enzi za Mh Mrema na kujiondoa kwake bungeni kipindi kile cha kashfa ya minofu ya samaki,chavda etc.This time mmeamua kui hande hii situation ya mafisadi in a different way,mathalan kutokuenda mahakamani na kuamua kutumia nguvu ya umma;hiyo ni baabkubwa kwasana kwasababu mmetumia mbinu ambayo serikali na ccm hawakuitarajia,wao walifikiri mtakimbilia mahakamni!So thats a very smart politics,cha muhimu ni kuendelea kuwa mtu mwenye principles kama ullivyosema na kuendeleza mapambano ya kweli kwa niaba ya wapena maendeleo.Kwa kushirikiana na Mh Mbowe na vichwa vingine ndani ya kambi ya upinzani nina uhakika its just a matter of time political revolution is within our reach.Tunataka Tanzania ambayo watu wanakuwa maarakani kulingana na sifa za kuwatumika wananchi na si yu tabaka flani,watu wenye maazo mapya na wenye kuweza kuletea chachu ya kimaendeleo na mageuzi ya kijamii na a kiuchumi.
Lstly tungependa utueleze pia kama utapitia Marekani kwenye ziara yako ya Canada.
God bless and MOST IMPORTANT;STAY SAFE!
J Mushi
9:28 PM
Kaka Zito nakupongeza kwa yote unayotutendea sisi watanzania,kwakweli unafanya mengi na ntakuwa mchoyo wa fadhila kama sitatambua hilo.
Nomba niseme moja kubwa kwamba nchi hii sio maskini kama inavyosemekana,ni aibu kubwa na kufuru kutamka kwamba eti Tanzania ni nchi maskini,tunamkufuru mungu.Hebu tafakari rasilimali tulizonazo na matumizi yake?,kwani mikoa kama KAGERA,MWANZA,SHINYANGA,MBEYA,RUKWA,SONGEA,MOROGORO,LINDI{SONGOSONGO},NA ARUSHA si ingeweza kabisaaa kukidhi yote Taifa hili inayohitaji?,NASIKITIKA SANA TUKISEMA ETI SIE MASKINI WAKATI Ardhi,madini yote mpaka gesi na mafuta tunayo,naomba nisiandike sana lakini nna machungu ntalia bure hapa.Ntablogu tena soon!!
4:37 PM
ndugu bwana Zitto, sidhani kama ni lazima ni lazima nikuandikie shairi kukusifu au kukupongeza kwa kuwa maandishi na sifa hazitasaidia kuainisha ukweli kuwa wewe ni kijana mheshimiwa wa kuigwa.nimekuwa nikifikiri kwa muda mrefu sana kama tunaweza kuwa na vijana wenzangu wenye mwamko kama ulionao.ninakupongeza sana kwa harakati zako na ujasiri ambao kwa kweli hata mimi ningetamani kutoukosa ninaungana na wewe mkono moja kwa moja ingawa ninaishi hapa ujerumani lakini bado tutapambana kuhakikisha taifa linakuwa kama ambavyo linatakiwa liwe na si kuburuzana.hongera sana kwa kutuamsha kuwa sasa ni wakati wa vijana hata kama itatugharimu kutoa maisha yetu kwa haki.
8:45 PM
Zitto... i play for you son i hope you will still stand for what you believe even when CCM millions come your way.
the truth is there will be no real change in Tanzania until us today people we sacrifice our life for our future generation...
when i say change i dont mean the new building and garden in dar-es -salaam. i mean education,water,health services,road,distribution of income and apportunities for all tanzania no matter the creed or color although manority tanzanian are the one who have it all by themself.Mo enterprise, radwa and co.
ill spend all my life time probably my kids too without Tanzania produce another JKN rip son of africa
9:27 AM
Mlalahoi naona umeshindwa kuwa objective kwa kazi ambayo kijana mwenzetu anaifanya maana katika comments zako huonyeshi unasimamia wapi katika comments. Zitto anafanya kazi nzuri na anastahili kupongezwa na kila mpenda haki na mpenda maendeleo ya nchi yake. Nina uhakika wewe huwezi kuwa frontliner kama alivyo Zitto. Hebu basi tuacknowledge his sacrifice ili ajue kwamba kazi yake haiendi bure bali kuna secret supporters ambao wako nyuma yake.
Mh. Zitto endelea na kazi uliyonayo na sisi tuko nyuma yako as a big army japo unaweza kuwa hulioni.
2:25 PM
Kwa kweli mimi binafsi bado sijajua msimamo wa chadema and what their overall agenda is.. but i have heard of you from family, news and friends and what you have done for tanzania so far..keep it up..
7:04 PM
kab
7:43 AM
Nipo nchini Marekani kwa muda wa wiki na nusu sasa. Nimetembelea miji ya Washington DC na New York. Nimefarijika sana na Watanzania walivyonikaribisha vizuri jijini Washington. Wamenipa heshima kubwa kutembelea majumbani kwao na pia kunialika katika sherehe ya Watanzania wanaoishi Maryland, Virginia na Washington DC. Ninaendelea na ziara yangu ambapo kuanzia jumapili nitakuwa Michigan ambapo nitakutana na Watanzania na pia nitaenda Hauston kutembelea ndugu na pia kukutana na ndugu zangu Watanzania.
7:48 AM
Post a Comment
<< Home