Blogu ya Mkurugenzi wa Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.

Monday, March 03, 2008

Kingunge alijivunjia mwenyewe heshima


Hebu nikukumbushe kauli zake kidoooooooooogo---

TAMKO KUHUSU KAULI ZA KINGUNGESisi, viongozi wa vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR Mageuzina TLP tuliokutana Equator Hotel tarehe 20 Septemba2007 hapa Arusha tumeitafakari “Orodha yaMafisadi”(List of Shame) na tumejadili kauli za Waziriwa Nchi, Ofisi ya Rais, Siasa na Uhusiano waJamii-Mheshimiwa Kingunge Ngombale-Mwiru alizozitoa 18Septemba 2007 na kunukuliwa na vyombo mbalimbali vyahabari Jumatano 19 Septemba 2007 na kwa pamojatumeazimia kutoa tamko lifuatalo:Kingunge anapotosha umma, apuuzwe; wapinzani wanateteataifaTunaunga mkono uamuzi wa viongozi wetu wa kitaifakuanika wazi kwa umma orodha ya mafisadi; hii ni kwasababu rasilimali zinazofujwa ni za wananchiwatanzania, wanaoathirika kutokana na ufisadi ni ummawa watanzania na wenye uamuzi wa mwisho wakuwawajibisha viongozi mafisadi ni umma wa watanzania.Kwa kuzunguka nchini kueleza yaliyotokea bungeni(hususani kusimamishwa kwa Mbunge Zitto Kabwe nakupigwa danadana kwa hoja ya kashfa ya ufisadi ndaniya Benki Kuu iliyokuwa iwasilishwe na Dr WilbroadSlaa) wakati wa Mkutano wa Bunge la Bajetiuliomalizika hivi karibuni, wabunge wa upinzaniwanatimiza wajibu wao kama wawakilishi wa kweli wawananchi. Kwa kuzunguka nchini kueleza kuhusu ufisadiunaendelea nchini, viongozi wa upinzani wanatekelezawajibu wao wa kisiasa wa kuwazungumzia wananchi wotewa Tanzania wanaoguswa na ufisadi bila kujali itikadiama uanachama; ikumbukwe kuwa vyama vya siasa siovyombo vya uchaguzi tu bali ni taasisi muhimu katikajamii katika kuchochea uwajibikaji na maendeleo. Kwamantiki hiyo basi Waziri Kingunge anaupotosha ummaanaposema kwamba ziara za viongozi wa upinzanizinatokana na ‘hasira ya kushindwa uchaguzi mkuu 2005,kambi ya upinzani kushindwa kumtetea Zitto bungeni,wivu wa kuona CCM inatekeleza ilani yake vizuri, nakwamba wanautumia vibaya mfumo wa vyama vingi’.Tunapenda kusisitiza kuwa Viongozi wa umma wanaokiukana/au kuvunja masharti ya katiba ya Jamhuri yaMuungano na Sheria za Maadili ya Viongozi wa ummalazima waanikwe hadharani na kuwajibishwa na yoyoteanayetoka kauli ya kubeza jitahada hizi ni vyemawatanzania wakampuuza. Kama viongozi wa upinzaniwanavunja sheria kwa kutoa uzushi na kufanya uchochezikama Waziri Kingunge anavyodai kwa nini serikalihaiwakamati na kuwapeleka mahakamani badala ya kutoamatamko ya kulalamika?Kauli za Kingunge ni msimamo wa Serikali?; Ikulu itoetamko!Tumezijadili kauli za Waziri Kingunge na katika hatuaya sasa tusingependa kuamini kama zinawakilishamsimamo wa serikali kwa ujumla wake; hatutaki kuaminikwamba kauli hizo ni msimamo wa pamoja wa Serikalichini ya Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekitiwa Baraza la Mawaziri. Katika hatua ya sasatunazichukulia kauli hizo kuwa ni maoni binafsi yaBwana Kingunge mpaka hapo Ikulu itakapothibitishavinginevyo; hivyo kwa tamko hili tungependa ikulu itoeufafanuzi kuhusu kauli hizo. Lakini tunapenda piakutoa tahadhari kwamba inawezekana kauli hizi za BwanaKingunge amezitoa kwa nia ya kupoteza lengo tuanzekuzijadili kauli zake badala ya kujadili orodha yamafisadi na hatma ya rasilimali za nchi yetu. Hivyotungependa kusisitiza kuwa ikulu ijibu hojazilizotolewa na viongozi wa upinzani ambazo zimemgusamoja kwa moja Rais na serikali.Anayelinda ufisadi ndiye anayekwamisha maendeleo nahuduma za kijamiiTunashangazwa na uamuzi kauli ya Kingunge kwambauamuzi wa Viongozi wa Vyama na Wabunge wa Upinzanikuzunguka nchini ni mkakati wa kisiasa wa kuitoaserikali kwenye mstari wa kushughulikia maji, afya nabarabara. Tunapenda kumbukusha Waziri Kingunge kuwakatika orodha hii ya mafisadi pekee zaidi ya shilingitrilioni 1.3(1,300,000,000,000) ambazo kamazingetumika vizuri ni wazi zingeweza kutumikakuboresha maji, umeme na barabara bila kuendeleakuwakamua zaidi wananchi masikini. Ukweli ni kuwa kwakuendelea kulea ufisadi serikali inajitoa yenyewekwenye mstari wa kutumia vyema kodi za wananchi narasilimali za taifa katika kushughulikia shughuli zamaendeleo na huduma za kijamii ikiwemo maji, afya nabarabara. Ni ukweli pia kwamba kwa kuwawajibishamafisadi viongozi wa upinzani wanatimiza wajibu wao wakuhakikisha rasilimali za taifa zinatumika kwa ustawiwa wananchi walio wengi.Vyombo vya dola tayari vinayo orodha ya mafisadi;vichukue hatuaTunashangazwa na kauli ya Waziri Kingunge ya kuhojisababu za Viongozi wa Upinzani kushindwa kuziwasilishakwenye vyombo vya dola tuhuma walizozitoa dhidi yavigogo hao iwapo kweli wanao ushahidi wakuzithibitisha. Tunashangazwa na kauli hii kwa kuwatunaamini kabisa Waziri Kingunge anafahamu kabisa kuwasehemu kubwa ya tuhuma hizi zipo katika Ripoti zaMkaguzi wa Serikali ikiwemo ile ya mwaka 2005/06 nakwamba vyombo vya dola vinafahamu uwepo wa tuhuma hizilakini kwa zaidi ya miaka miwili vyombo hivyohavijachukua hatua dhidi ya vigogo waliotajwa.Tunaamini kwamba viongozi wa upinzani walichofanya nikuamua kushtaki kwa wenye mali walioibiwa ambao niwananchi wote wa Tanzania ili kwa pamoja tuwezekuvitaka vyombo vya dola viweze kuchukua hatua.Tunashangazwa na kauli hii ya Waziri Kingunge ya‘kuwahukumu’ viongozi wa upinzani kwa kushindwakupeleka ushahidi kwa kuwa kauli hii inapingana nakauli zingine ambazo zimewahi kutolewa na viongozi waserikali kuhusu tuhuma hizo hizo. Tunapendakumkumbusha Waziri Kingunge kwamba tayari Spika WaBunge-Samuel Sitta alishasema kwamba anavipelekapolisi vielelezo vyote vya ushahidi alivyotoa Dr Slaaili vichunguzwe. Pengine Kingunge angetoa hukumu hiyokwa Spika kwa kushindwa kupeleka vielelezo. Piaikumbukwe kwamba ni serikali hiyo hiyo iliyowahi kutoataarifa kwa umma kwamba tuhuma za ufisadi ikiwemo zaBOT zinachunguzwa na TAKUKURU. Kadhalika WaziriMkuu-Edward Lowasa alitoa kauli baadaye kwambaSerikali iliyafahamu madai ya Kashfa ya ufisadi BenkiKuu(BOT) kabla ya upinzani. Kwa upande mwingine, madaiya kutaka kushughulikia rushwa kubwa kubwa ikiwemo zakwenye mikataba yalianza kutolewa na Rais Kikwetewakati akifungua Mkutano wa Kwanza kabisa wa Bungemwaka 2005. Lakini baadaye ni Rais Kikwete alinukuliwana vyombo vya habari akisema kwamba anawafahamu walarushwa na anawapa muda wajirekebishe; tulitarajiaWaziri Kingunge kama mshauri wa Rais wa masuala yasiasa angemshauri apeleke ushahidi katika vyombo vyadola na si kuwahukumu viongozi wa upinzani ambaowametoa orodha ya mafisadi na ushahidi kutoka kwenyetaasisi za serikali yenyewe!. Na ni jukumu la vyombovya dola kuchukua hatua za kufuatilia baada ya orodhaya mafisadi kuwekwa hadharani.TAKUKURU inajipotezea imani yenyewe!Tumeshangazwa pia na kauli ya Waziri Kingunge yakuwalaumu viongozi wa upinzani kwa kutokuwa na imanina TAKUKURU. Kwa misingi ya kauli zao ambazo wamezitoakatika nyakati mbalimbali, viongozi wa upinzaniwamekuwa wakikisisitiza kuwa TAKUKURU inajipotezeayenyewe imani kwa wananchi kutokana na taarifa zake nakwamba wamekuwa wakiipa changamoto TAKUKURU kuchukuahatua. Mathalani TAKURU kuisafisha kampuni yaRICHMOND. “….hakuna ushahidi wowote uliopatikanakuthibitisha vitendo vya rushwa, uzembe na upokeaji wakamisheni watendaji wa serikali….uchunguzi huoumethibitisha udhaifu wa kawaida katika utendaji naambao haukuhusisha rushwa au manufaa ya aina yoyoteile kwa upande wa watendaji na hakuna hasarailiyosababishwa na udhaifu huo”(Mwananchi 12/5/2007).“….baada ya kuona hivyo, Richmond ilionekana kufahamumwenendo wa mambo serikalini…”(Tanzania Daima12/5/2007). Maswali yaliyobaki mpaka hivi sasa ambayosi TAKURU wala TAKUKURU ya sasa hawajayajibu ni pamojana: Ni kwanini Kamati ya Waziri Mkuu iliipa tendaRichmond baada ya Bodi ya Wakurugenzi ya Tanescokuitaka bodi yake ya sabuni kutangaza upya zabuni hiyokwa kutimia zabuni za kimataifa? Richmond kuwezakufahamu mwenendo wa mambo ya ndani serikalini sioishara ya rushwa ya kimadaraka? Ni kweli kama hakunahasara iliyosababishwa na uamuzi huu wakati ambapowatanzania wamekaa bila umeme kwa miezi mingi bilakupata umeme wa dharura waliotarajia wakati wadharura, Rais amekiri kwamba umeme ulichangia kushukakwa kasi ya ukuaji wa uchumi na hata kuongeza mfumukowa bei na mpaka leo bado megawatts 100 hazijatimizwana Richmond/Dowans? Tunapenda kumkumbusha WaziriKingunge kwamba Mkataba wa Richmond/Dowans pekeeumeligharimu taifa zaidi ya Bilioni 200 mpaka sasaambazo zingeweza kuelekezwa kwenye elimu, afya nabarabara. Viongozi wa upinzani wanapohoji utendaji waTAKUKURU wanataka ichukue hatua za harakakushughulikia mafisadi na kuendelea kuwa Taasisi yaKuzuia na Kudhibiti Rushwa na si Taasisi ya Kulinda,Kusafisha ama Kutetea Rushwa !Wasomi na asasi za kijamii wako sahihi; Kingungeamelewa madarakaTumefadhaishwa na kauli ya Waziri Kingunge kwambawasomi nchini wametathimini uamuzi wa Bunge wakumsimamisha Mbunge Zitto Kabwe kwa kutanguliza jazbabadala ya busara na kutilia wasiwasi uelewa wa makundiya kijamii kuhusu mantiki ya uzalendo. Hatutakikuamini katika hatua ya sasa kwamba huu ni msimamo waserikali kwamba wasomi na makundi ya kijamiiwametanguliza jazba na kukosa busara na uelewa katikakuijadili adhabu aliyopewa Mbunge Zitto Kabwe na hojayake ya kutetea Rasilimali za nchi yetu hususanimadini. Tunaamini kwamba kauli hii ni maoni binafsi yaBwana Kingunge ambayo ni ishara ya kulewa madarakakutokana kung’ang’ania serikalini toka wakati nchi hiiinapata uhuru kwani hii si mara ya kwanza kutoa kauliza kubeza-aliwahi kuibeza CHADEMA kwa kumtaja Nyererekwenye kampeni 2005 na hivi karibuni Julai 3, 2007aliripotiwa na vyombo vya habari akitetea msimamo waRais Kikwete wa kutumia nafasi yake kama raiskudhoofisha upinzani kwa kufanya kampeni za CCM katikamikutano ya kiserikali. Tunapenda kumbukusha WaziriKingunge maneno ya Shaban Robert kwamba “ elimuilipokuwa bado kujulikana mvi zilihesabika kuwa alamaya hekima lakini fikra hizo wakati wake umeshapitahaupo na wala hauji tena. Kisichobadilika ni kwambamtu mzima bado anastahili heshima kutoka kwa mdogo” .Ni vyema Waziri Kingunge akafahamu kwamba wasomi kamaProfesa Issa Shivji na makundi ya Kijamii mathalaniMtandano wa Jinsia(TGNP), Chama cha Wanasheria waMazingira(LEAT), Kituo cha Sheria na Haki zaBinadamu(LHRC) walifanya tathmini yao kwa lengo lakulinda maslahi ya taifa bila kujali itikadi.Mafisadi zaidi waendelee kutajwa; serikali ijibu hojaHivyo tunapongeza na tutaendelea kuunga mkono jitahadazote za vyama vya siasa, asasi za kijamii na hata watubinafsi waliowataja na watakaoendelea kuwatajaviongozi na/au maafisa wa umma na/au mawakala na/auwashirika wao katika sekta binafsi ambao kwa namnambali mbali wameshiriki katika kupora utajiri na/aufedha za umma na hivyo kulisababishia taifa na umma waWatanzania ufukara na/au umaskini mkubwa. Kadhalikatunaunga mkono na kutoa mwito kwa vyama vya siasa,asasi za kijamii na hata watu binafsi kuendeleakuwawajibisha viongozi wa umma ambao kwa kutumianyadhifa na/au vyeo vyao katika utumishi wa ummawamefanya maamuzi ambayo yamesababisha taifalimepoteza mapato na/au utajiri na rasilmali zake nakuwaneemesha raia na/au taasisi za kiuchumi na/au zakibiashara za kigeni. Kwa mfano, viongozi wa ummawalioshiriki katika kusaini mikataba mibovu katikasekta za madini na/au nishati na/au maeneo mengineyenye umuhimu mkubwa kwa maisha ya taifa na jamii yaWatanzania. Na katika haya tunataka serikali ijibuhoja na si kupuuzia na kutoa kauli za kejeli kama "haoni wapinzani hawana jingine la kufanya", "wana haki yakutoa maoni yao na huo ndio uzuri wa demokrasia" .Waziri Kingunge na serikali kumbukeni kuwa watuwachache wanaweza kudanganyika katika muda mchachelakini watu wote hawewezi kudanganywa wakati wote.Watanzania wa leo na kesho si watanzania wa jana najuzi.John MnyikaMkurugenzi wa Vijana Taifa (CHADEMA)Na Mwenyekiti wa KikaoGodbless LemaKatibu Mwenezi Mkoa-Arusha(TLP)Na Msemaji wa Ushirikiano wa Vyama vya Upinzani-ArushaMohamed MaabadMwenyekiti wa Wilaya-Arusha Mjini(CUF)Na Mwenyekiti wa Ushirikiano wa Vyama vyaUpinzani-ArushaEned MuroMwakilishi-Arusha(NCCR-Mageuzi)Amos KibandaKatibu Mkoa-Arusha(CHADEMA)Calist LazaroMwenyekiti wa wilaya-Arusha Mjini (TLP)